Idara ya uhusiano na vyuo vikuu yahitimisha ratiba ya hema la sita kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq…

Maoni katika picha
Jioni ya Juma Nne (2 Dhulhijja 1439h) sawa na (14 Agosti 2018m) hema la sita liitwalo (Hema la marehem Ibrahim Mutayyam) la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq limehitimisha ratiba yake, chini ya mahudhurio makubwa ya wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu, pamoja na ugeni wa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ratiba hii ya hema ni miongoni mwa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ya kuhitimisha ratiba hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa jengo la Imamu Haadi (a.s), ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na mwanafunzi Ali Hamdani, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na ustadh Azhar Rikabi, ambaye alibainisha kua: “Wazo la kwanza la kuanzishwa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel lilianza mwaka 2010m, tulizingatia mazingira ya kazi na mahitaji ya vyuo, leo hii tumesha jifunza namna gani tutachukua fikra za chuo na fikra za wanachuo kupitia wanachuo wanao ishi mabwenini na kuziendeleza, mafanikio tuliyo pata ndani ya miaka hii ni fahari kubwa pamoja na idadi ndogo ya watalamu katika kitengo cha mahusiano na vyuo vikuu, tumepata mafanikio makubwa, mafanikio hayo yanatokana na msaada mkubwa kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na ndugu zetu wapambananji”.

Baada ya ujumbe huo ukafuata ujumbe wa wanafunzi washiriki ulio wasilishwa na mwanafunzi Akram Aaridhi ambaye alisema kua: “Hema hili ni sehemu zinapo kutana nyoyo za kweli, na kituo cha kuendeleza vipaji vyetu na kuonyesha uwezo wetu, hema hili ni sawa na kioo tunacho tumia kuangalia nafsi zetu, na kujuana na marafiki kutoka katika vyuo vikuu tofauti, sisi hapa kupitia msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu ni wanafunzi tulio ungana kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali vya Iraq chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, mradi ambao umetoa kundi la wahitimu ambao leo hii ni wakufunzi katika vyuo vikuu vya Iraq”.

Akaoneza kua: “Hakika mradi huu unalenga kuandaa viongozi wa taifa, mradi huu unahusisha mihadhara ya kukuza uwezo wa kibinadamu, mihadhara kuhusu mbinu za mawasiliano ya kiofisi pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua, mihadhaya ya kufundisha uzalendo wa taifa na kulipenda kwa kuzingatia historia yake na uzuri wa tamaduni zake, na kujipanga kwa ajili ya kujenga mustakbali bora, unao endana na utukufu wa taifa hili, hali kadhalika hema hili lilihusisha mihadhara ya dini kutoka kwa viongozi wa hauza, kuhusu namna ya kupambana na changamoto za kiimani na zinginezo, pamoja na visomo vya Qur’an na kutembelea malalo matakatifu, pia tulitambulishwa vitengo vya Ataba tukufu pamoja na majukumu ya kila kitengo, na washiriki ni wanafunzi wa vyuo vikuu tofauti vya Iraq”.

Halafu yakafuata mashairi yaliyo somwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika ratiba ya hema, hafla ikahitimishwa kwa maelezo ya makamo rais wa kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Abdulkarim Shaami, na ujumbe wa Ustadh Jasaam Saidi ambaye ni kiongozi wa idara ya habari za kimataifa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alielezea miradi mikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na miradi midogo midogo na huduma zinazo tolewa na Ataba tukufu katika jamii kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: