Marjaa dini mkuu: Raia wa Iraq wanamaadili mema na akili pevu kila mtu anatakiwa kunufaika na hilo na tuunde jamii iliyo elimika…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu amebainisha kua raia wa Iraq wana maadili mema na akili pevu, kila mtu anatakiwa kunufaika na hilo na tuunde jamii iliyo elimika, na tuwe na vijana wanao elewa mambo kwa undani.

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) Ijumaa ya leo (5 Dhulhijja 1439h) sawa na (17 Agosti 2018m) iliyo ongozwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Mabwana na mabibi siku za nyuma tuliongelea kuhusu mtu anaye toa huduma, tukataja baadhi ya mambo yanayo endana na swala hilo, kisha tukataja hasira na athari chanya katika kutetea haki, leo tunazungumzia mada nyingine muhimu ambayo inahusu utamaduni kwa ujumla au kusoma.

Bila shaka kusoma ni miongoni mwa mambo matukufu na hupevusha muono, mwanadamu anapo kua na utamaduni fulani bila shaka atakaua sehemu ya utamaduni huo, na utamaduni huo utakua sawa na kinga baina yake na manbo mabaya yanayo weza kutokea au yakumtoa katika njia sahihi, kawaida ujinga ndio husababisha kuharibika kwa jamii yeyote, na ujinga haupendezi kwa jamii yeyote, atakapokua baba wa familia hajui namna ya kuongoza familia yake bila shaka familia hiyo haitakua na mwisho mwema, kila ujinga unavyo kua mkubwa ndio madhara yanavyo kua makubwa, nitazungumzia baadhi ya mambo ya kijamii.

Mwanadamu hupata wapi maarifa? Utamaduni huupata wapi? Hujifunza kutoka wapi? Lazima kuwe na vyanzo vinavyo aminika kwake ili mwanadamu aweze kujifunza, na viwe vyanzo vinavyo aminika wakati wote na kila mahala, mtu anaye taka kujifundisha hutakiwa avumilie shida na tamaduni hua hazikosekani.

Mwanadamu anapo iandaa nafsi yake kwa ajili ya kusoma japo kidogo, anatakiwa apambane na mapungufu ya nafsi yake, ujinga wakati wote husababisha mtu afanye mambo yasiyo kua mazuri, nataja mfano mdogo, -simaanishi kumbeza yeyote kwa mfano huu-, tiba ni miongoni mwa mambo muhimu, na kutibu miili ni muhimu sana, unaweza kukuta taktari anahangaika kumtibu mgonjwa akiwa na lengo la kumfundisha mgonjwa namna ya kutunza afya yake, mgonjwa akijua utunzaji wa afya yake hatakwenda mara kwa mara kwa daktari kwa samabu maradhi yatapungua, kwani atajiepusha na vitu vingi vyenye madhara naye, wakati mwingine daktari hafurahii kumuona mgonjwa anafahamu jinsi ya kutunza afya yake, kwani kuendelea kutojua jinsi ya kulinda afya yake ni bora kwake, kama akiwa hajui kulinda afya atanufaika naye zaidi kwa sababu ataugua mara kwa mara na atakwenda kwa daktari mara kwa mara na daktari atanufaika naye kwa muda mrefu.

Mimi nazungumzia mazingira hayo tu na siwalengi madaktari –naomba mnielewe vizuri- katika kila jamii, nani anaye wajibika kuelimisha jamii? Je kuna watu maalumu wanao wajibika? Je ni wanasiasa au taasisi za kiraia, na nani anye wajibika kuelimisha watu? Mimi kama mwanadamu nawajibika kujielimisha na kujiendeleza, nitakapo kua situmii uwezo wangu katika njia sahihi, nitakua na mwenendo mbaya, na nitaweza kuambukiza mabaya yangu kwa watu wengine.

Baadhi ya watoto wetu unapo ongea nao unaona namna walivyo changanikiwa, kwa sababu wanaiga utamaduni mpaya, wanajifunza kupitia mitandao ya kijamii na wanaamini kila wanacho kiona huko, wanakifanyia kazi na kuwafundisha wengine, hili sio jambo zuri, jambo muhimu zaidi kila mtu amepewa akili, Mwenyezi Mungu mtukufu ameifanya akili kuwa kitu maalumu kwetu wanadamu, akili huisimamia nafsi na inatambua kila inacho fanya itaulizwa, Qur’an inasema (Wasimamisheni. Hakika wao watasailiwa) na katika aya nyingine inasema (Hakika masikio, na macho, na moyo hivyo vyote vitasailiwa).

Kwa ajili ya kujali watoto wetu, jitahidi kutumia vizuri akili ili ikufikishe mahala pazuri, kuwa mwenye kujifunza na uangalie unajifunza wapi, usiwe mjinga unakariri unayo soma na unasambaza unayo sikia, sitaki kuingia katika mambo mengine, lakini kuna baadhi za siasa zina ujinga kidogo, kama vile kuna ladha fulani ya kubakiza mazingira katika hali hii ya kutojitambua, mtu mwenye elimu hutambua mambo mengi na anaweza kukataa mengi anayo ambiwa, kwa hiyo kukaa bila elimu kuna manufaa kwa watu wengine.

Jamii ya raia wa Iraq ni nzuri, na vijana lazima wawe na utamaduni mzuri, lazima tupambane na ujinga, sisemi nani mwenye jukumu hilo bali ni jukumu la kila mtu, mimi na wewe, vyombo vya habari na baba wa familia, hili sio jambo la kisiasa bali nijambo la kijamii, na likiachwa ni hatari, raia wa Iraq ni wema na wana akili pevu, watu wote, familia, wanawake, wanaume wanatakiwa kunufaika na hili na kujenga jamii iliyo elimika, iliyo soma kwa undani sio wanao nakili na kusema, utukufu wa mwanadamu huonekana kutokana na kauli zake.

Kuna mtu mmoja alikaa mbele ya mfalme, mfale akamuambia: Ongea nifahamu uzito wako kupitia maneno yako, ujinga unatakiwa umalizwe, mwalimu anawajibika na wahadhiri pia wanawajibika, mtu anae tafuta kitu fulani hujihisi mapungufu hadi apate kitu hicho, pia anatakiwa akitafute kwa kutumia njia sahihi na vyanzo bora, ikhtilafu, uzushi na uongo havikubaliki, Mitume na waja wema walikadhibishwa, kukusudia kudanganya watu ambao wataamini uongo wako na watausambaza kwa watu wengine huku wakijua kua wanasema kweli, ni kujiingiza katika tatizo lingine, pamoja na kujipoteza wewe mwenyewe lakini unapoteza na watu wengine, ninaamini kua hili jambo ni muhimu sana, wala sitaki kuelezea zaidi ya nilivyo sema, lakini lazima tupambane kuondoa ujinga, mtu anapo taka kuihami nafsi yake anatakiwa asome japo kidogo.

Mwenyezi Mungu atufundishe yanayo tufaa duniani na akhera, na akuhifadhini na kila baya, na mwisho wa maombi yetu husema kila sifa njema anastahiki Mola Mlezi wa walimwengu, na rehma na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na Aali wake watakasifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: