Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea na semina za kiangazi na yapanda mbegu ya uwelewa wa Qur’an na maadili ya kiislamu katika nyoyo za mabinti...

Maoni katika picha
Mradi wa semina za Qur’an za majira ya kiangazi kwa wasichana, ni moja kati ya miradi muhimu inayo yanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, semina hizo zinafanywa katika makao makuu yaliyopo Najafu na katika matawi, bado semina zinaendelea, zinapata mwitikio mkubwa kutoka kwa mabinti wenye umri wa miaka kumi na moja hadi wale waliopo vyuoni, wamezifanya semina hizi kua fursa kwao ya kuongeza uwezo wao katika Qur’an na kunufaika na kipindi cha likizo, mwaka huu semina hizi zimekua na ongezeko kubwa la washiriki sambamba na kuongeza maeneo ya semina.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa Maahadi wamesema kua, hakika semina za Qur’an zilizo anza mwanzoni mwa likizo za kiangazi zinavipengele vingi vinavyo lenga kufundisha maadili mema kwa mabinti, na kuwapa malezi sahihi ya kiislamu yanayo endana na mafundisho ya dini yetu tukufu pamoja na mwenendo wa Mtume mtukufu (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s).

Hakika semina hizi zina masomo yaliyo pangiliwa na wabobezi wa Qur’an, ambapo wanafundishwa usomaji, hukumu na njia za kuhifadhi Qur’an, pamoja na masomo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaq yanayo endana na umri wa washiriki, ambao wamepangwa kulingana na umri wao kuanzia wale wanao soma darasa ya tano shule za msingi hadi wale wanaosoma vyuo, hali kadhalika semina hii inakipengele cha kuwafundisha kazi za mikono.

Kumbuka kua semina hii inafanyiwa katika tawi la Maahadi katika mkoa wa Najafu Ashrafu, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mahitaji ya lazima yote, kuanzia nakala za Qur’an hadi usafiri bure, semina imepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa mabinti na wameichukulia kuwa fursa ya kukuza uwezo wao wa Qur’an na kunufaika na kipindi cha likizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: