Kamati ya misaada ambayo ipo chini ya ofisi ya Sayyid Sistani yatoa misaada kwa wakazi wa kijiji cha Haudh Hamrin…

Maoni katika picha
Bado mkono wa kheri unao nyooshwa na kamati ya misaada ambayo ipo chini ya ofisi ya Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Sistani unaendelea kusaidia kila anaye hitaji msaada, mkono huu wa kibinadamu umesha fika katika mikoa mingi ya Iraq toka wakati wa mwanzo kabisa ilipo tolewa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu ya kuilinda Iraq na maeneo yake matukufu na kuanza kupatikana wakimbizi, ulikua dawa ya majeraha yao na uliweza kupunguza matatizo yao na kuwasaidia kupambana na mitihani, baada ya Mwenyezi Mungu kutupa neema ya ushindi, kamati bado inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu, na mara hii imefunga safari hadi katika kijiji cha Haudh Hamrin kilichopa katika njia inayo elekea mpakani mwa mji wa Matwibija wanako ishi watu wa ukoo wa Shammar, Uzzah na Abiid.

Rais wa kamati Sayyid Shahiid Mussawi ametuambia kua: “Baada ya kufika maombi ya kuhitaji msaada katika ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani, kamati yetu imekuja kutoa msaada kwa wakazi wa kijiji hiki, ambao wameanza kurubi baada ya kukombolewa kwake kutoka katika mikono ya magaidi wa Daesh, tumekua tukifanya hivi tangu kuanza kupatikana wakimbizi, kwa maombi kutoka kwao au bila maombi, tunaratiba kamili ambayo imeorodhesha maeneo na muda tunayo tumia katika ugawaji wa misaada, tutaendelea kutoa misaada hadi mkimbizi wa mwisho atakapo rudi nyumbani kwake”.

Akaongeza kua: “Msaada huu umehusisha vikapu vya chakula (2000) elfu mbili, vikiwa na aina nane za vyakula, pamoja na nguo za watoto (2500) za aina mbalimbali, zilizo gawiwa kwa familia zinazo rudi majumbani kwao zikiwa na mazingira magumu, kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na kikosi cha (21) cha Hashdi Sha’abi”.

Akabainisha kua: “Wakazi wa kijiji hicho walikua na furaha kubwa sana iliyo onekana wazi katika nyuso zao, walimshukuru sana Mheshimiwa Marjaa dini mkuu, kwa sababu hakuwasahau wakati walipo sahauliwa na kila mtu, katika kuonyesha furaha yao waliichukulia siku ya kuwapa misaada kua ni sikukuu yao, kwa sababu ugeni wa ofisi ya Marjaa upo pamoja nao na unawajulia hali zao”.

Kumbuka kua misafara ya kugawa misaada inayo fanywa na kamati hii bado inaendelea chini ya ratiba maalumu katika hema za wakimbizi au katika miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kupunguza machungu ya familia hizo na kuwafanya wahisi kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wairaq wote bila kujali tabaka zao na mielekeo yao, na kuondoa picha mbaya inayo sambazwa na maadui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: