Kumbukumbu iumizayo: Mwezi saba Dhulhijja alifariki Mpupia elimu na Imamu muongoaji Muhammad bun Ali (a.s)…

Maoni katika picha
Mwezi saba Dhulhijja ni siku ya huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) siku iumizayo zaidi kwao na kwa wapenzi wao, ni siku aliyo fariki Imamu wa tano katika Maimamu wa nyumba ya Mtume na mtu aliye fanana zaidi na Mtume (s.a.w.w) ambaye ni Imamu Muhammad Baaqir (a.s) mpupiaji wa elimu na Imamu muongoaji, kiongozi wa wacha Mungu na mteule katika waja, ni bendera ya minara na hazina ya hekima za Mwenyezi Mungu na mfasiri wa wahyi.

Imamu Baaqir (a.s) aliuawa kwa sumu aliyo pewa na Khalifa wa bani Umayya Hisham bu Abdulmalik, aliyo iweka katika tandiko la farasi aliyo pandishwa Imamu (a.s) –na inasemekana aliinywa katika kinywaji-, alifanikisha uovu wake huo wakati wa kumrudisha Imamu Madina kutoka Damaskas baada ya kumwita (huko) Sham, Imamu (a.s) alifariki siku ya Juma Tatu mwezi saba Dhulhijja mwaka wa (114h) katika mji wa Madina, akafariki (a.s) kwa sumu akiwa ni mwenye kufanyiwa dhulma, na akazikwa katika makaburi ya Baqii katika mji wa Madina, sehemu alipo zikwa Abbasi bun Abdulmutwalib, pia ndio sehemu alipo zikwa baba yake Imamu Sajjaad (a.s) na ndugu wa baba yake Imamu Hassan Almujtaba (a.s), tena ni karibu na bibi yake Fatuma bint Asad mama wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Imamu Swadiq (a.s) amesema kuhusu baba yake Imamu Baaqir (a.s) kua siku ya kufa kwake alisema: (Usiku huu nitaondoka katika dunia hii, nimemuona mzazi wangu –akukusudia Imamu Sajjaad (a.s)- ameniletea kinywaji kitamu nikanywa, akanipa bishara ya kuingia katika nyumba ya milele na kukutana na haki).

Miongoni mwa mabo ya pekee kwa Imamu huyu, ameunganisha familia ya Imamu Hussein na Imamu Hassan, ni Hasimiyyu wa kwanza kuzaliwa upande wa Hassan na Hussein (a.s), baba yake ni Ali bun Hussein na mama yake ni Fatuma bint Hassan (a.s), hivyo alikua ni makutano ya karama na kipenzi cha Alawiyya, kuzaliwa kwake ilikua furaha kubwa sana kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) hakika utukufu wake hauelezeki.

Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kua alisema: (Hussein atakapo ondoka duniani, kiongozi baada yake atakua ni mwanaye Ali yeye ni hoja na ni Imamu, na Mwenyezi Mungu atatoa kutoka katika mgongo wa Ali mtoto jina lake linafanana na jina langu na elimu yake sawa na elimu yangu, anafanana sana na mimi naye ni Imamu na hoja baada ya baba yake).

Imepokewa kuwa Imamu Sajjaad (a.s) alimuambia mwanaye Baaqir (a.s) kua: (Mwanangu mimi nakufanya kua kuongozi baada yangu, yeyeto atakaye puuza hili Mwenyezi Mungu atamvisha taji la moto siku ya kiyama).

Imamu Baaqir (a.s) alikua ni bahari ya elimu, alikua na elimu ya hali ya juu kabisa hakuna yeyote anaye mkaribia, ndio maana akaitwa (Mpupia elimu), zama zake zilijaa mijadala ya kielimu, kwa sababu utawala wa bani Ummayya ulifungua milango ya kuanzishwa kwa madhehebu potofu, uzushi na mielekeo miovu, hivyo Imamu Baaqir (a.s) akasimama imara kupambana na fikra potofu na kuwaelekeza katika njia sahihi.

Lakini pia viongozi wa bani Umayya walikua wanamuogopa sana kutokana na heshima kubwa aliyo kuwa anapewa na wanachuoni pamoja na watu wa kawaida, na hawakupata sababu ya kumbana Imamu (a.s), ndio wakalazimika kumuua kwa siri kwa kutumia sumu, umma ukamkosa Imamu atokanaye na kizazi cha Mtume (s.a.w.w) tawi imara miongoni mwa matawi ya mti mtakatifu, amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo fariki na siku atakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: