Mawakibu za kuomboleza zamiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kuwapa pole kutokana ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Baaqir (a.s)…

Maoni katika picha
Tangu mapema asubuhi kama kawaida yao katika siku kama hizi za huzuni zilizo umiza moyo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Baaqir (a.s), malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) yamefurika mawakibu za waombolezaji za hapa Karbala, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu hii inayo uma, na kufanyia kazi kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amemrehemu atakaye huisha mambo yetu), na kuangazia kumbukumbu hii chungu kwa kushiriki katika kuwapa pole watu wa nyumba ya Mtume kutokana na msiba huu walio pata katika siku kama ya leo sambamba na kubainisha kudhulumiwa kwao.

Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu maombolezo haya kua: “Hakika mawakibu za waombolezaji katika matukio ya vifo vya Maimamu (a.s) huanza kuwasiri mapema, likiwemo tukio la kumbukumbu ya kifo cha Imamu Baaqir (a.s), hii ndio aina ya uombolezaji iliyo zoweleka tangu zamani, watumishi wa kitengo chetu huratibu matembezi yao, mawakibu huingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia mlango wa Kibla na baada ya kutoa pole, huelekea katika malalo ya muhusika mkuu wa msiba na baba wa maimamu watakasifu (a.s) Abu Abdillahi (a.s) wakipitia katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, katika matembezi hayo hushiriki pia kundi la mazuwaru”.

Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hufanya maombolezo ya msiba huu –wa kifo cha Imamu Baaqir (a.s)- kila kona ya dunia, kumbukumbu ya msiba huu unasadifu siku ya (7 Dhulhijja) ndio siku aliyo fariki (a.s) kwa sumu aliyo pewa na khalifa wa utawala wa bani Umayya Hisham bun Abdulmalik ambayo iliwekwa katika tandiko la farasi aliyo pandishwa Imamu (a.s) –na inasemekanya aliinywa katika kinywaji-, alitekeleza uovu huo wakati alipo mrudisha Imamu katika mji wa Madina baada ya kumwita Sham, Imamu (a.s) akafariki siku ya Juma Tatu mwezi saba Dhulhijja mwaka wa (114h) katika mji wa Madina, akafariki kwa sumu akiwa kadhulumiwa, na akazikwa katika makaburi ya Baqii ndani ya mji wa Madina, katika sehemu alipo zikwa Abbasi bun Abdulmutwalib na baba yake Sajjaad na ndugu wa baba yake Hassan Almujtaba (a.s) pia ni karibu na sehemu alipo zikwa bibi yake Fatuma bint Asadi mama wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: