Mwezi nane Dhulhijja.. Imamu Hussein (a.s) abadilisha Ihram ya hija na kufanya Umra ya peke yake kisha aelekea Iraq…

Maoni katika picha
Harakati ya Imamu Hussein (a.s) ilipitia hatua nyingi, na kuifanya kua harakati ya milele ambayo nuru yake itaendelea kuangazia na kuongoza watu, miongoni mwa hatua za harakati hiyo, ni pale alipo ongoka Makka na kwenda Iraq, ambapo; hapo awali aliuacha mji wa babu yake Mtume (s.a.w.w) na kwenda Makka, (siku aliyo ondoka Makka kwenda Iraq) ilikua ni mwezi nane Dhulhijja mwaka (60h) siku ya kunywesha maji (Tarwiyya).

Imamu Hussein (a.s) alipo uacha mji wa babu yake Mtume (s.a.w.w) na kwenda Makka hakua na nia ya kukaa Makka moja kwa moja, bali alipanga kupafanya kua kituo cha harakati yake, akae kwa muda fulani kisha aendelee na safari ya kwenda Iraq.

Kutokana na barua nyingi za watu wa mji wa Kufa zilizo tumwa kwa Imamu Hussein (a.s) akiwa Makka, aliamua kumtuma mjumbe wake huko Kufa, akamteua mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s), aende kuandaa mazingira, (Muslim bun Aqiil –a.s-) alipo fika katika mji wa Kufa, watu wa mji huo walikula kiapo cha utii kwa Imamu Hussein (a.s), naye aliwaelezea viongozi wa Kufa malengo ya harakati ya Imamu Hussein (a.s), wote walitangaza utiifu wao kwa Imamu Hussein (a.s), katika mazingira hayo mazuri Muslim bun Aqiil akamuandikia barua Imamu Hussein (a.s) ya kumuhimiza aje katika mji wa Kufa.

Imamu Hussein (a.s) akapata barua ya Muslim bun Aqiil, iliyo muelezea mazingira ya kisiasa na namna anavyo kubalika na watu wa Iraq, Imamu (a.s) akaondoka Makka siku ya Juma Nne mwezi nane Dhulhijja kuelekea Iraq, akiwa na watu themanini na mbili miongoni mwa wafuasi wake na watu wa nyumbani kwake kabla ya kumaliza ibada ya hijja, inamanisha kua Imamu (a.s) hakumaliza ibada ya hijja kutokana na mazingira magumu yaliyo kuwepo, na ili aende kutekeleza wajibu wa kisheria na kiuongozi, Imamu Hussein (a.s) aliwakusanya wake zake, watoto wake, ndugu zake, watoto wa ndugu zake, watoto wa ammi zake, na wakaanza safari ya kuondoka Makka tukufu.

Imamu Hussein (a.s) akaondoka Makka, huku Yazidi bun Muawiyya (lana iwe juu yake) akamtuma Amru bun Said bun Aaswi kutoka Madina kwenda Makka akiwa na askari wengi ili aende kumkamata Imamu Hussein kwa siri, na akishindwa kumkamata basi amuue hata kama atakua ameshika pazia za Kaaba, Imamu Hussein (a.s) alipojua njama hiyo, aliacha ibada ya Hijja na akafanya Umra ya peke yake na akaondoka kwenda Iraq, kutokana na kuogopa asiuawe ndani ya Kaaba na kuvunja heshima ya Kaaba tukufu, kwani Yazidi haogopi kufanya uovu huo, Imamu (a.s) akamuambia ndugu yake Muhammad bun Hanafiyya: (Ewe ndugu yangu naogopa Yazidi bun Muawiya asiniuwie ndani ya Kaaba tukufu, nikawa sababu ya kuvunjiwa heshima nyumba hii).

Siku ya kuondoka kwake katika mji wa Makka alitoa khutuba mashuhuri isemayo: (Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na kila atakalo hua wala hakuna nguvu ispokua zake, na rehma na amani ziwe juu ya Mtume wake… Mauti yameandikwa kwa mwanadamu ni kama mkufu aliovaa shingoni, nina shauku nayo kama shauku ya Yaquub kwa Yusufu, na nitapata kifo bora zaidi, kana kwamba nipo katikati ya mbwa mwitu jangwani baina ya Nawasisi na Karbala, na kuliwa na wanyama pori, hakuna njia ya kukwepa jambo lililo andikwa, ridhaa ya Mwenyezi Mungu ni ridhaa yetu Ahlulbait, tunasubiri katika mitihani yake, na anatulipa malipo ya wenye kufanya subira, hatuta enda kinyume na Mtume wa Mwenyezi Mungu bali tutakusanyika kwake katika hadhira ya utukufu, na kufurahisha macho, na kutekeleza ahadi yake, ambae yupo tayali kujitolea kwa ajili yetu, na nafsi yake iko tayali kukutana na Mwenyezi Mungu, asafiri pamoja nasi, hakika mimi nasafiri kesho ashubuhi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: