Inatokea hivi sasa: Kuanza ibada za siku ya Arafa ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika uwanja wa katikati yao…

Maoni katika picha
Ndani ya eneo tukufu na watu waliojaa imani tangu saa saba Adhuhuri ya leo (9 Dhulhijja 1439h) sawa na (21 Agosti 2018m) zimeanza ibada za siku ya Arafa katika malalo matukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu. Uwanja uliopo katikati ya haram mbili umefurika mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, walianza kumiminika katika eneo hilo tukufu tangu jana usiku, ibada zimeanza kwa kusomwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zilizo somwa na Muhammad Lutufi, kisha ikafuata dua ya siku ya Arafa ya Imamu Hussein (a.s) iliyo samwa na Shekh Ahmadi Duru Al-Aamiliy pamoja na dua zingine.

Kwa upande mwingine; viwanja vya malalo mawili matukufu, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) yameshuhudia ibada za mtu mmoja mmoja, kwa ajili ya kuhakikisha sehemu hizo zinaingia idadi kubwa zaidi ya watu, pia viwanja vilivyopo jirani na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya vimejaa mazuwaru wanaofanya ibada mmoja mmoja au kwa vikundi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha jipanga kuimarisha usalama na kutoa huduma bora kwa kutumia nguvu zake zote ili kuhakikisha ziara na ibada hizi zinafanyika kwa amani na utulivu bila bugudha yeyote.

Tunapenda kufahamisha kua kituo cha uzalishaji wa vipindi na utangazaji wa moja kwa moja kimeandaa masafa maalumu ya bure kwa ajili ya kurusha ibada hizi moja kwa moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: