Kwa picha: Chini ya ulinzi mkali na huduma bora waumini wafurika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kufanya ziara na ibada za Arafa…

Maoni katika picha
Wanatofautiana lugha zao na milengo yao lakini wanakubaliana katika jambo moja nalo ni kumpenda Imamu Hussein (a.s) na kuwepo kwao Karbala, kielelezo cha kupambana na madhalimu na sehemu iliyo shuhudia ushindi wa damu dhidi ya upanga, katika mazingira bora ya kiroho ndani ya eneo tukufu la Kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Ataba tukufu za Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Adhuhuri ya leo zimeshuhudia mafuriko makubwa ya waumini waliokuja kufanya ziara na ibada za siku hii tukufu ya Arafa.

Wamekuja kutafuta utukufu wa kuhudhuria katika ardhi ya Karbala siku ya Arafa, ulio elezwa katika hadithi tukufu, kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu huangalia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kabla ya kuangalia mazuwaru wa Arafa katika mji mtukufu wa Makka.. mkutano bora kiasi gani! Hongera yao wale watakao ridhiwa na muumba wao, ni kuangaliwa kwema.. kwa Karbala na Makka.

Mahudhurio haya matukufu sio ya wairaq peke yao, bali kuna mazuwaru wengi wamekuja kutoka nje ya Iraq katika nchi za kiarabu na kiislamu, hakika watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya kila wawezalo kuhakikisha wanaondoa kila aina ya uzito kwa mazuwaru na kuwawezesha kufanya ibada kwa amani na utulivu, vikundi vya watoa huduma vimeenea katika njia zote zinazo elekea katika haram mbili tukufu kwa ajili ya kutoa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: