Kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kimefanya kazi kubwa katika kipindi cha ziara ya siku ya Arafa na siku ya Idil Adh-ha…

Maoni katika picha
Kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimefanya kazi kubwa katika kuwapokea mazuwaru wa siku ya Arafa na siku ya Idil Adh-ha tukufu, kimefanya kila kiwezalo kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibada kwa amani na utulivu na kiliandaa vitu vyote muhimu vinavyo hitajika.

Rais wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Bwana Adnani Ni’matu-Dhaifu amesema kua: “Maandalizi ya ziara hii tukufu yalianza siku kadhaa kwa kushirikiana na idara zote za kitengo hiki, kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa maandalizi tuliyo fanya ni:

  • - Kutandika miswala eneo lote la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
  • - Kuhakikisha maji baridi ya kunywa yanapatikana saa (24) kwani yanahitajiwa na mazuwaru kutokana na kuongezeka kiwango cha joto.
  • - Kuwasha feni zinazo puliza na kurashia maji kwa ajili ya kupunguza kiwango cha joto.
  • - Kuhakikisha mitambo ya kufanyia usafi inafanya kazi muda wote kwa ajili ya kudhibiti usafi wa eneo hili.
  • - Kuhakikisha watumishi wa kitengo hiki na wale wa kujitolea wapo kila mahala kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mazuwaru watukufu.
  • - Kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kurusha ibada za ziara katika siku ya Arafa.
  • - Kusambaza turba na viti vya kuswalia wenye mahitaji maalumu na wazee.
  • - Kusambaza idadi kubwa ya vitabu vya ziara na dua.
  • - Kuweka njia maalumu za kuingia na kutoka kwa ajili ya kudhibiti msongamano wa watembeaji.
  • - Kusambaza miamvuli ya ziada kwa ajili ya kujikinga na jua”.

Akabainisha kua: “Watumishi wa kitengo hiki wanauzowefu mkubwa wa namna ya kuwahudumia mazuwaru wengi, walio pata katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kila idara ilipewa majukumu kutokana na nafasi yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: