Makumi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq vya nufaika na masafa ya bure iliyo tengenezwa na kituo cha utengenezaji wa vipindi na matangazo ya moja kwa moja…

Maoni katika picha
Kituo cha utengenezaji wa vipindi na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua, makumi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq vimenufaika na masafa waliyo tengeneza, ambayo ilitumika kurusha ziara na ibada za Arafa bure, pamoja na swala ya Idil Adh-ha tukufu iliyo swaliwa katika haram mbili, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili sambamba na vionjo vya kitaalamu vilivyo ingizwa wakati wa matangazo.

Mkuu wa kitengo Ustadh Bashiri Taajir akaongeza kusema kua: “Siku baada ya siku tunaona maendeleo ya wazi katika sekta ya urushaji wa matangazo unaofanywa na kituo cha Alkafeel, haya ni matokeo ya uzowefu walionao watumishi wa kitengo hiki kuanzia wapiga picha hadi watengenezaji wa vipindi, pamoja na ubora wa vifaa walivyo navyo, mambo yote hayo yamesaidia kupatikana kwa picha bora zinazo kubalika na vyombo vya habari na kukidhi mahitaji yao, kwa hiyo masafa inayo toa matangazo bure imekua kimbilio kwa vyombo vya habari vinavyo penda kurusha ibada na ziara ya Arafa mubashara (moja kwa moja)”.

Akabainisha kua: “Hakika masafa hiyo ni ya Atabatu Abbasiyya tukufu nayo imetoa ushirikiano kwa vyombo vingine vya habari kwa kuelekeza magari yao ya matangazo ya moja kwa moja pamoja na watalamu wao, picha zilikua zinapatikana bila tatizo lolote na walikua na uhuru wa kuzitumia watakavyo”.

Kumbuka kua kituo cha utengenezaji wa vipindi na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel kinamiliki masafa maalum inayo toa matangazo bure chini ya taratibu maalumu, masafa hiyo inapatikana kupitia anuani zifuatazo:

SAT:INTELSAT 902@62°E
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
8PSK
FEC 2/3
HD/MPEG-4
Unaweza kufuatilia matangazo ya moja kwa moja au kupakua kupitia youtube kwa anuani ifuatayo:

https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw

Au kwa kupitia facebook kwa anuani ifuatayo:

https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: