Kwa mara ya kwanza katika historia ya Iraq na kati ya nchi (130): Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya imehudhuria katika kongamano kubwa la kimataifa la maktaba na taaluma…

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika kongamano la kimataifa la themanini na nne linalo husu maktaba na taaluma, lililo andaliwa na umoja wa vikundi na taasisi za maktaba (Ifla) katika mji mkuu wa Malezia Kwalalumpa kuanzia tarehe (24) hadi (30) mwenzi huu wa nane, chini ya kauli mbiu isemayo (Kubadilisha mwenendo wa maktaba ni njia ya kubadilisha jamii), ambalo linalenga kuangalia nafasi ya athari za maktaba katika kubadilisha jamii na umma na kuleta maendeleo.

Hii ni mara ya kwanza kwa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kushiriki katika kongamano hili la kimataifa na ni taasisi pekee kutoka Iraq inayo shiriki, hii ni fursa ya kubainisha utendaji wake na kuangalia maendeleo ya kielimu yaliyopo katika maktaba za kimataifa, kutokana na msingi huo ilikubali kuhudhuria na kushiriki na itakua ni nafasi nzuri ya kuonyesha walicho nacho na kuangalia wengine wanafanya nini pamoja na kuonyesha picha kua Iraq ni nchi ya elimu pamoja na mazingira magumu inayo pitia.

Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika hafla ya ufunguzi ulio fanyika asubuhi ya leo (24/08/2018m) na kufunguliwa na bibi Karsi Oliva mkuu wa bunge pamoja na baadhi ya (RDA), amezungumzia umoja wa wajumbe wa (RDA) katika kongamano hili na kubadilishana uzowefu baina yao, ameelezea uzowefu kutoka nchi mbalimbali duniani huku akiangazia (RDA) kua inanafasi nyingi za kuchukua uzowefu katika maktaba kote duniani, miongoni mwake maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kuangalia uzowefu wa wengine katika sekta hii, imechaguliwa kua miongoni mwa nchi (30) zitakazo zungumza katika kongamano hili kuhusu: (Nafasi ya maktaba za Iraq baada ya Daesh), hii ni nafasi muhimu sana kwa maktaba za Iraq.

Kumbuka kua kongamono hili (Ifla) linamada nyingi, na linahudhuriwa na wasomi wengi walio bobea katika mambo ya maktaba kutoka kila sehemu ya dunia na hufanywa kila mwaka, huratibiwa na taasisi za maktaba na taaluma wanachama wa (Ifla), pamoja na jumuiya ya maktaba za Malezia, na hufadhiliwa na wizara ya utalii na utamaduni ya Malezia pamoja na maktaba za malezia, (MYCEB), ushiriki wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho na kongamano hili ni wa mara ya kwanza kwa taasisi za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: