Hafla ya kufunga semina imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Shekh Kuleaini (r.a) na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na ilikua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na uwasilishaji wa ujumbe kutoka kwa washiriki, ulio wasilishwa na Zaharaa Ali Saalim mmoja wa washiriki wa semina, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kufanya semina hizi muhimu tulizo nufaika nazo, na tutayafanyia kazi katika maisha yetu yale tuliyo soma kwenye semina hizi, akatoa shukrani pia kwa wazazi na walezi wa mabinti walio shiriki kwa kuwaruhusu mabinti zao kuja kushiriki, pia akawashukuru sana wasimamizi wa semina kwa kazi kubwa waliyo fanya katika kipindi chote cha semina.
Hali kadhalika katika hafla hii kulikua na vipindi vya kaswida na mashairi na mwisho kabisa wanasemina wakapewa vyeti vya ushiriki, na wasimamizi wa semina wakapewa vyeti vya kupongezwa.
Makamo kiongozi mkuu wa idara tajwa hapo juu Ustadhat Taghridi Abdul-Khaaliq Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Semina hizi zimepangwa ili kuhakikisha kipindi cha likizo za kiangazi kinatumiwa vizuri na kunufaika nacho, tuliandaa ratiba maalumu kwa kila rika, na tukawawekea masomo yanayo endana na viwango vyao na yanayo husu mazingira halisi waliyo nayo, baada ya kuwagawa katika vikundi chini ya walimu wenye uzowefu mkubwa wa shughuli hizi, semina ilikua na mwitikio mkubwa sana, masomo yaliendelea kila siku katika ukumbi wa chini (Sardabu ya Imamu Kadhim -a.s-), Atabatu Abbasiyya tukufu iligharamia usafiri wa washiriki kuwatoa majumbani kwao na kuwarudisha kila siku”.
Akaongeza kua: “Ratiba ilikua na masomo mengi miongoni mwa masomo hayo ni:
- - Masomo na mihadhara tofauti.
- - Usomaji sahihi wa Qur’an pamoja na tafsiri za baadhi za aya kwa kusherehesha na aya zingine pamoja na haditi za Mtume.
- - Historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuangalia hadithi zao sambamba na kuzilinganisha na hali halisi tunayo ishi hivi sasa.
- - Masomo ya Fiqhi na Aqida yanayo endana na rika zao.
- - Masomo ya fani ya ushairi na uwasilishaji.
- - Vipengele mbalimbali”.