Marjaa dini mkuu amebainisha kua wajibu wa kibinadamu na kitaifa na kisheria unawataka viongozi wahusika washirikiane kuweka ukomo wa matatizo ya watu wa Basra, upatikane haraka ufumbuzi wa matatizo yao, swala hili linawezekana kama kukiwa na nia ya kweli kwa viongozi wa serikali kuu na serikali ya mkoa.
Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (12 Dhulhijja 1439h) sawa na (24 Agosti 2018m) iliyo swaliwa katika uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) na kuongozwa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, amesema kua:
Bado watu wa Basra wanaendelea kulalamikia matatizo makubwa waliyo nayo ya ukosefu wa maji safi ya kunywa, na ukosefu mkubwa wa maji hata ya kuoga na matumizi mengine ya kibinadamu, kutokana na ukosefu wa maji baadhi ya wakazi hutumia maji machafu ambayo huwasababishia maradhi ya ngozi, pamoja na kuzungumzwa jambo hili na Marjaa dini sambamba na vyombo vingine lakini juhudi zinazo fanywa za kutatua tatizo hili bado hazionyeshi tatizo litaisha lini, inasikitisha sana kuona tatizo hili la kibinadamu halipewi umuhimu unao faa na viongozi wa serikali wanao husika zaidi ya kutumiana lawama wao kwa wao na kila mmoja kuonyesha mapungufu ya mwenzake katika hili, hakika wajibu wa kibinadamu na kitaifa na kisheria unazitaka pande zinazo husika kushirikiana na kuweka ukomo wa kutatua matatizo ya watu wa Basra, upatikane ufumbuzi wa haraka, jambo hili linawezekana kama wote wakiwa na nia za kweli kuanzia uongozi wa serikali kuu na serikali ya mkoa, na wakafanya kazi kwa timu ya kutatua kero za wananchi haraka na kuacha marumbano baina yao.