Atabatu Abbasiyya tukufu yawakaribisha na kuwakirimu zaidi ya mayatima (1000)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa utaratibu wake wa kujenga uhusiano mwema na taasisi tofauti za nje, hususan taasisi zinazo lea mayatima na mafakiri ili kuwafanya wahisi malezi ya ubaba, na kwa ajili ya kuchangia furaha katika maisha yao na kukamilisha furaha ya sikukuu tukufu ya Idil Adh-ha, Atabatu Abbasiyya tukufu imewakaribisha zaidi ya mayatima (1000) walio chini ya taasisi ya Imamu Sajjaad (a.s) Alkhairiyya, ya kuozesha vijana na kulea mayatima katika mkoa wa Karbala.

Baada ya kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) walifanya mazungumzo yaliyo husisha wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya pamoja na uwakilishi maalumu wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pia kulikua na mawaidha yaliyo tolewa na Sayyid Adnani Mussawi kutoka katika kitengo cha dini ambaye alibainisha kua: “Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake kitukufu kua: (Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri), wakati mwingine tunapewa mitihani ya kupungukiwa mali au watu na matunda, katika taifa letu la Iraq tumepewa mtihani ya mambo haya matano, sasa hivi tupo na watu mlio pewa mtihani wa kupungukiwa na watu, kuna wajane na mayatima tunao wahudumia, tutapambana namna gani na mtihani huu? Bila shaka ndugu zangu namna ya kupambana na mtihani kunahitaji subira, ndio tumepata mtihani huu je ndio mwisho wetu? Je tutasema yanayo mkasirisha Mwenyezi Mungu? Tunatakiwa kupambana na mtihani kwa kufanya subira, mwanamke aliye poteza mumewe akawa mjane na mtoto aliye poteza baba wote wanatakiwa kuwa na subira, Mwenyezi Mungu anawajali sana mayatima na sio sisi, sisi tunatekeleza maagizo ya Mwenyezi Mungu mtukufu kuwatumikia watu walio poteza wapenzi wao na wakapoteza wahudumu wao kwa hakika wanahitaji kusaidiwa”.

Sayyid Fadhil Husseini ambaye ni rais wa taasisi ya Imamu Sajjaad (a.s) Alkhairiyya, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mayatima walio chini ya taasisi yetu wamezoa kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na viongozi wake kila mwaka katika siku ya pili ya Idil Adh-ha, hufanya ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha hula chakula cha mchana pamoja na kupewa zawadi za Idi, hii sio mara ya kwanza kukirimiwa mayatima na Atabatu Abbasiyya tukufu, ni mwendelezo wa kuwafurahisha mayatima na kushiriki pamoja nao katika furaha”.

Mayatima na walezi wao pia wamezungumzia furaha kubwa waliyo nayo kutokana na ukarimu walio fanyiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku hizi tukufu.

Mayatima walifuatana na Ustadh Sa’adi-dini Hashim Mahdi ambaye ni mkuu wa ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu ambaye alisema kua: “Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kipindi chote umekua ukionyesha kuwajali na kuwathamini mayatima na walezi wao, na jambo hili la kuwakirimu mayatima na walezi wao tumelifanya katika siku hizi tukufu za Idil Adh-ha, Atabatu Abbasiyya tukufu imekaribisha idadi kubwa ya mayatima na walezi wao takriban watu elfu moja na kuwakarim, ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula katika mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s), huduma hizi endelevu zinatokana na maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na sio katika siku za sikukuu peke yake bali katika kipindi chote cha mwaka”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaratiba nyingi kuhusu vikundi vya kijamii, miongoni mwa vikundi hivyo ni mayatima na watu wanao ishi katika mazingira magumu, imekua ikiyafanya haya kwa ajili ya kuwashirikisha mayatima katika jamii, na kupunguza hali ya unyonge wanayo ishi nayo asilimia kubwa ya mayatima kwa sababu ya uyatima wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: