Makumbusho ya Alkafeel yatoa mafunzo kwa watumishi wake ya utengenezaji wa miswala ya makumbusho kwa ufundi wa zamani wa darizi za kihindi…

Maoni katika picha
Watumishi wa makumbusho ya vifaa na nakala kale Alkafeel ya Atabatu Abbasiyya tukufu hawajatosheka na ufundi wa kutengeneza miswala ya makumbusho pekeyake, bali wamepanua wigo zaidi kutokana na watalamu walio nao na hamu ya kutaka kujua vitu vingine, watumishi hao wameingia katika semina ya kujifundisha kutengeneza miswala kwa kutumia mikono.

Tumeongea na rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim kuhusu mafunzo haya, naye kasema kua: “Miongoni mwa utaratibu wa kuongeza ujuzi kwa watumishi wa makumbusho ya vifaa na nakala kale Alkafeel, makumbusho imeandaa semina ya kumi na mbili ya kutengeneza miswala kwa mikono, nayo ni miongoni mwa semina inayo husu vitu tofauti vya makumbusho, kwa kua miswala ina nafasi kubwa tumeipa kipao mbele zaidi, mafunzo haya yanalenga kuinua uwezo wa watumishi wetu katika sekta hii na kulinda ufundi huu usipotee, pamoja na kuenzi ufundi wa kutengeneza miswala kwa mikono, hakika mafunzo haya yanayo simamiwa na Ustadh Masudi Haidari yanamada nyingi kuhusu hatua na vifaa vinavyo tumika katika kutengeneza miswala, na namna ya kuandaa mchoro na kufanya usanifu kisha kuingia hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza kwa mikono hadi uwe mswala kamili”.

Kwa upande mwingine, watumishi wa makumbusho kutokana na uwezo walio pamoja na ufundi wa darizi za kihindi, ambazo ni fani za zamani zilizo fanywa na watu wa kale kwa kuweka picha za kiislamu, elimu hii imechukuliwa kutoka katika kitambaa cha zamani kilicho dariziwa kwa uzi wa madini na kutiwa nakshi za mapambo ya mimea na kiislamu, kilitolewa uzi ulio kua umepandana na ukakazwa kwa kutumia uzi na singano, kisha kikawekewa kitambaa cha katani na kushonewa juu yake, baada ya kukiweka kitambaa cha katani katika maji kwa ajili ya kuondoa uchafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: