Baada ya kuusafisha na kuurekebisha, kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kazi ya kuurudisha katika hali yake ya kawaida, kutoka katika mazingira ya kutupiwa taka hadi katika muonekano mzuri wa kuburudisha familia zinazo ishi karibu yake, kwa kuupalilia na kuweka mawe ya mapambo pamoja na kupanda mauwa yanayo ongeza uzuri wa muonekano.
Mkuu wa utekelezaji wa mradi huu ambaye ni rais wa kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Bwana Khaliil Hanuun ametuambia kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya miradi mingi katika mji wa Karbala, kwa ajili ya kuuendeleza na kuupendezesha, ukiwemo mradi huu wa kuusafisha mto wa Hunaidiyya, ambao sio mto tu, bali ni sawa na roho inayo zunguka katika mitaa ya mji, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa watu wanao ishi pembezoni mwa mto huo, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kuurudisha katika muonekano mzuri, kwa kufanya kazi ya kuupalilia na kuweka vivuko, kupanda mauwa na kuweka mapambo pamoja na mambo mengine mengi, kazi hii inafanyika kwa kushirikiana na idara ya maji pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa na wataalamu wa kitengo chetu wenye uzowefu na uwezo mkubwa wa kufanya miradi ya aina hii”.
Akaongeza kua: “Kazi hii ilitanguliwa na kazi zingine nyingi, miongoni mwa kazi hizo ni: Kufanya utafiti na kubaini njia ya mjo, kisha ukaandaliwa mpango kazi ambao uligawa vipengele vya utendaji katika hatua tofauti, hatua ya kwanza ilikua ni ya kusafisha mita mia moja upande wa barabara ya Muhammad Amiin, ambapo baada yake ndio utekelezaji wa mradi wa kutengeneza eneo la mto lenye urefu wa (km 3) chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukaanza”.
Akabainisha kua: “Kazi za awali zilikua ni:
- - Kupalilia mto na kuusafisha kwa kuondoa magugu na taka zote.
- - Kuweka mawe katika mto pamoja na aina tofauti za mapambo.
- - Kuweka vivuko juu ya mto ili iwe rahisi kwenda upande wa pili.
- - Kutengeneza sehemu za maporomoko ya maji pembezoni mwa mto.
- - Kuweka mtandao wa taa za kisasa.
- - Kupanda miti ya muta mrefu na ya muda mfupi pembezoni mwa mto.
- - Kuweka meza na viti pembezoni mwa mto.
- - Kuifunika ardhi kwa Kashi za mawe”.
Hanuun akamaliza kwa kusema kua: “Kazi inaendelea vizuri, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu tunatarajia kumaliza ndani ya muda ulio pangwa na kwa ubora mkubwa, mto huu utarudia katika uzuri wake tena ukiwa na muonekano mpya na kua moja ya sehemu nzuri za kupumzika hususan kwa wale wano ishi pembezoni mwa mto huu na kwa yeyote atakaye penda kuja kupumzika”.