Kujiandaa na mwaka mpya wa masomo: Kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu chaanza ujenzi wa mabweni ya ziada ya wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Ameed…

Maoni katika picha
Kutokana na kujiandaa na mwaka mpya wa masomo na kujipanga kupokea idadi kubwa ya wanafunzi wa kike pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri, na kuwapunguzia kazi wazazi wao ya kuwatafutia makazi bora na salama nje ya chuo, kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza ujenzi wa mabweni ya wasichana katika chuo kikuu cha Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Muhandisi Abbasi Mussawi amesema kua: “Ujenzi huu unafanyika ndani ya eneo la chuo, katika uwanja wenye ukubwa wa mita za mraba (1113) chengo hili litachukua zaidi ya wanafunzi (144), vyumba vitawekwa vifaa vyote muhimu kwa wanafunzi, pia kutakua na kumbi za kujisomea pamoja na kumbi za kulia chakula na jiko kubwa sambamba na eneo la vyoo lenye kila kitu kinacho hitajika, tunatarajia kumaliza ujenzi kabla ya kuanza muhula ujao wa masomo, hivyo litakua tayali kupokea wanafunzi wa muhula ujao”.

Uongozi wa chuo umesema kua: “Mradi huu unapewa umuhimu mkubwa na chuo kikuu cha Ameed, kutokana na kukaribia kipindi cha usajili wa wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo, chuo kina jukumu la kujali jambo hili, mwaka ulio pita tulipokea idadi kubwa ya wanafunzi kutoka mikoa tofauti ya Iraq, jambo ambalo linatulazimu kuandaa mabweni mengine kwa ajili ya kupokea wanafunzi wapya, ili wasipate usumbufu wa kutafuta makazi nje ya chuo, watakaa bure bila malipo ya ziada zaidi ya ada zao za masomo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: