Miongoni mwa orodha ya turathi za Hilla zilizo hakikiwa: Kituo cha turathi za Hilla chatoa kitabu kipya kiitwacho: (Mafaqihi wakubwa na maendeleo ya harakati za kifikra katika mji wa Hilla)…

Maoni katika picha
Mji wa Hilla una nafasi kubwa katika turathi za Iraq, hasa turathi za kiislamu na za dini zito zilizo toka mbinguni kwa ujumla, mji wa Hilla unahistoria kubwa imeelezewa na mamia ya vitabu vya histori, adabu, rijaal, jografia na vinginevyo.

Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu –miongoni mwa kazi zake- ni kuandika vitabu kuhusu turathi, wameandaa milango na faharasi kwa kuangalia mada za turathi chini ya usimamizi wa kamati ya watu walio bobea katika fani hii, miongoni mwa orodha ya matoleo yao ni tolea la turathi za Hilla zilizo hakikiwa ambalo limetoka hivi karibuni katika kitabu kiitwacho: (Mafaqihi wakubwa na maendeleo ya harakati za kifikra katika mji wa Hilla) kilichopo katika juzuu mbili, kilicho andikwa na Alammah Sayyid Haadi Hamdu Aali Kamali-Dini Alhusseiniy Alhilliy mwaka (1405h), na kufanyiwa uhakiki na Dokta Ali Abbasi Alawiy Al-A’arajiy.

Kumbuka kua kuanzishwa kwa kituo cha turathi za Hilla, kumetokana na harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya elimu na utafiti, na kusaidia kuibua historia za miji ya Iraq, na kikaunganishwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, nacho ni miongoni mwa vituo vilivyo funguliwa katika miji tofauti ya Iraq, kwa ajili ya kulinda turathi za miji hiyo na kuandika vitabu sambamba na kufanya utafiti wa kina wa turathi zilizopo katika miji hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: