Mradi wa majengo ya chuo katika mkoa wa Najafu: Ujenzi unaendelea na umekamilika kwa kiasi kikubwa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi inayo pewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni mradi wa majengo ya chuo unaojengwa katika mkoa wa Najafu, kitakua na vitivo kadhaa, chuo hicho kinajengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya (80,000), panatarajiwa kua kitovu cha elimu na kuchuana na vituo vya aina hiyo vya kitaifa na kimataifa kutokana na masomo yatakayo fundishwa pia kutokana na aina ya ujenzi wake, kitafanya kazi kwa kufuata vigezo vya kimataifa na kuchuana na vyuo vikuu vingi kwa ubora wa kimasomo na uwezo wa kufanya utafiti wa kielimu, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh.

Akaongeza kusema kua: “Ujenzi unaendelea vizuri chini ya utaratibu ulio pangwa tunatarajia kumaliza mapema vitivo viwili miongoni mwa vitivo vya chuo hiki, navyo ni kitivo cha udaktari wa meno na kitivo cha Famasia, ambavyo kila kimoja kinaukubwa wa mita za mraba (1,700) na jengo la ghorofa nne, zikiwa na vyumba vya madarasa, maabara na ofisi za watendaji, majengo ya vitivo hivyo yanatarajiwa kufunguliwa mwaka huu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na tutaendelea na ujenzi wa vitivo vingine kama ilivyo pangwa, kiwango cha ukamilifu katika majengo ya vitivo viwili hivyo kimefika asilimia themanini (%80).

Akabainisha kua: “Ujenzi huu unafanyika sambamba na kazi zingine ambazo pia zimekamilika kwa kiasi kikubwa, kama vile ujenzi wa nyumba za chini na ufungaji wa mtandao wa zima moto, ujenzi wa vyoo, ufungaji wa umeme na uwekaji wa mtandao wa maji safi ya kunywa, hali kadhalika wameanza kutengeneza njia na kazi zingine ambazo zinafanyika pamoja na kazi hizi”.

Akasisitiza kua: “Majengo yote kuanzia ya chuo na yanayo husiana na chuo yanajengwa kwa kufuata vigezo vya wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu”.

Akaendelea kusema: “Hakika mradi huu unamalengo mengi miongoni mwa malengo yake ni:

  • - Kubaini vipaji vya wairaq na kuangalia namna ya kunufaika navyo.
  • - Kutengeneza mazingira bora ya ufaulu na kuandaa ratiba inayo endana na viwango vya taasisi za elimu za kisekula za kimataifa.
  • - Kuandaa nafasi za kazi kwa wasiokua na kazi kutokana na uwezo wa chuo.
  • - Kupunguza msongamano wa wanafunzi katika vyuo vikuu binafsi na vya serikali.
  • - Kwenda sambamba na maendeleo ya kielimu yaliyopo katika sekta za elimu kinadhariyya na kivitendo kwa kufuata utaratibu maalumu.

Kumbuka kua ujenzi wa chuo hiki upo ndani ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo lenga kuinua kiwango cha elimu hapa nchini, na kwenda pamoja na maendeleo ya kielimu yanayo tokea duniani, baada ya kumaliza ujenzi wa taasisi za malezi na elimu sasa hivi unafanyika ujenzi wa majukumu ya taasisi hizo za malezi na elimu, moja kati ya mambo muhimu ni ujenzi wa vyuo na huu ni mwanzo wa mwelekeo sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: