Miongoni mwa bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Aljuud ni mbolea inayo tokana na uoto wa baharini yenye uwezo mkubwa wa kuongeza mavuno…

Maoni katika picha
Mbolea zinazo tengelezwa na shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud inatokana na uoto wa baharini kwa (%100) ni mchanganyo wenye uwezo mkubwa wa kustawisha mmea katika hatua zote, imechanganywa na vichocheo asilia zaidi ya (30) pia ina (K2O 4% - P2O5 4% - N 4%).

Inavichocheo kuzia vya asili pamoja na (manganese – Magnesium – calcium – zinc – boron – iron – Sulfur – copper).

Wakulima wanatumia kiasi kikubwa cha mbolea hii kila mwaka, kutokana na umuhimu wake katika kustawisha mimea kwani ina vichocheo vikubwa na vidogo, na huiwezesha mimea kupambana na hali ngumu ya mazingira ya ukame na chumvi.

Mbolea hii itokanayo na uoto wa baharini inasaidia sana kurutubisha ardhi kwa mujibu wa wanafizikia na kemia na inauwezo mkubwa wa kutunza unyevunyevu, pia huubakiza mmea katika muonekano mzuri kwa muda mrefu, inakuza miche haraka na matunda au mimea iliyo samadiwa kwa mbolea hii hukaa muda mrefu bila kuharibika, inafaa kutumiwa katika hatua zote za ukuaji wa mmea.

Miongoni mwa faida za mbolea hii ni:

  • Huongeza uwezo wa utendaji wa mizizi.
  • Huuwezesha mmea kustahamili mazingira ya chunvi nyingi.
  • Huwezesha mmea kustahamili mazingira ya joto kali.
  • Huongeza kinga ya mmea.
  • Huongeza umri wa mavuno kwa mmea na kutoa mazao bora yanayo pendwa sokoni.

Kumbuka kua bidhaa hii imetengenezwa na raia wa Iraq na imekidhi vigezo vyote vya ubora, imethibitisha ubora wake katika vipimo na katika uwanja wa kazi (shambani) kwa kustawisha mazao zaidi, mbolea hiyo inapatikana katika vituo vya mauzo ya moja kwa moja vilivyo chini ya shirika hili katika mkoa wa Karbala na nje ya mkoa huo, kwa maelezo zaidi biga simu namba (07801930125 au 07801035422) au tembelea kituo cha mauzo kilichopo katika barabara ya (Najafu/ Karbala) mkabala na nguzo namba (1145).

Fahamu kua kwa sasa shirika limetoa aina nne za mbolea hiyo na linatarajia kuongeza aina zingine, aina zilizopo ni:

  • 1- Mbolea itokanayo na uoto wa baharini (ALgazone Delta 4).
  • 2- Mbolea itokanayo na uoto wa baharini (ALgazone potassium plus).
  • 3- Mbolea itokanayo na uoto wa baharini (ALgazone Evergreen).
  • 4- Mbolea itokanayo na uoto wa baharini (ALgazone MX30).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: