Chuo kikuu cha Al-Ameed chatangaza kuanza usajili wa wanafunzi wa kiarabu na kiajemi katika vitivo vyake…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza usajili wa wanafunzi wa kiarabu na kiajemi wasio kua raia wa Iraq katika vitivo vyake vya (Utaktari, Udaktari wa meno na Uuguzi) chini ya vigezo vilivyo pasishwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu kitengo cha vyuo binafsi na vya kigeni.

Chuo kimetangaza kwa kila anayetaka kujiunga aangalie vigezo na kujaza fomu katika toghuti ifuatayo: http://alameed.edu.iq/ au afike katika majengo ya chuo yaliyopo katika mkoa mtukufu wa Karbala, barabara ya (Karbala – Najafu) mkabala na nguzo namba (1238).

Kumbuka kua chuo kikuu cha Al-Ameed ni taasisi ya kielimu ambayo ipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kimesha idhinishwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kilianzishwa ili kiwe kituo cha elimu sambamba na vyuo vikuu vingine, kinatumia mfumo wa kimataifa unaokiwezesha kua miongoni mwa vyuo tegemezi, chuo kipo katika mkoa wa Karbala mwanzoni mwa barabara ya Karbala – Najafu, karibu na nguzo namba (1238), kwa maelezo zaidi unaweza kubiga simu ifuatayo (07602403019) au tuma barua pepe kupitia anuani hii (info@alameed.iq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: