Atabatu Kadhimiyya tukufu yashuhudia uwekaji wa madirisha mawili la Shekh Mufiid na Khawaja Tusi…

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wa kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha na milango ya malalo matukufu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na watumishi wa kitengo cha makenika cha Atabatu Kadhimiyya tukufu wameanza kazi ya kuweka madirisha mawili ya wanachuoni wakubwa, dirisha la Shekh Mufiid na Khawaja Nasrudini Tusi katika haram ya Kadhimiyya.

Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Kadhimiyya na mjumbe wa kamati iliyo simamia utengenezwaji wa madirisha hayo Bwana Qassim Kashkuul wameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunashuhudia kuwekwa madirisha mawili yaliyo tengenezwa kwa makubaliano baina ya uongozi mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, yaliyo fanyika mwezi kumi na nne Ramadhani mwaka 1438h, baada ya kupatikana kwa uwezo na uzowefu mkubwa katika kiwanda cha Saqaa unaoshinda nchi zilizo endelea katika utengenezaji huu”.

Akaongeza kua: “Kulikua na juhudi za wazi zilizo fanywa na kamati wakati kazi ya utengenezaji wa madirisha inaendelea, na kulikua na majadiliano mbalimbali kuhusu kulinda madhumuni ya madilisha hayo, na mapambo yake zikiwemo aya za Qur’an tukufu na maneno ya beti za mashairi, sina cha kusema zaidi ya kutoa shukrani kwa kazi kubwa iliyo fanyika hadi kukamilika kwa mradi huu”.

Upande wake mjumbe wa kamati ya watengenezaji wa madirisha hayo kutoka katika kiwanda cha Saqaa Ustadh Ali Saffaar amesema kua: “Kazi hii tukufu imefanywa na raia wa Iraq kwa (%100), sehemu ya nane ya kiwanda cha Saqaa ilishuhudia usanifu na utengenezaji wa madirisha haya mawili ambayo yanakila aina ya uzuri, miongoni mwa uzuri wa madirisha haya ni: uchaguzi wa mapambo na nakshi nzuri zilizo pelekea kupendeza zaidi kwa huu muonekano mpya, pamoja na kutumiwa mafundi waliobobea katika uselemala na wabobezi wa hati kwa ajili ya kuandika aya za Qur’an na hadithi tukufu pamoja na beti za mashairi ambazo zimepamba madirisha hayo matukufu, hati ya Thuluth ndio iliyo tumika kuandikia aya za Qur’an tukufu, pia madirisha hayo yanaendana na majengo ya Atabatu Kadhimiyya tukufu, leo hii tunafuraha kubwa sana kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) hadi katika haram ya Maimamu wawili Jawaadain (a.s) kuja kuweka madirisha haya”.

Tambua kua uzinduzi wa madirisha haya utafanyika siku chache zijazo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Tunapenda kusema kua watalamu wa kiwanda cha Saqaa wamekua na mafanikio mfululizo katika utengenezaji wa madirisha ya makaburi matukufu na mazaru, tangu walipo fanikiwa kutengeneza dirisha la kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha wakatengeneza mlango wa Hamdi wa malalo ya Sayyid Muhammad –Sab’u Dujail- (a.s), na leo hii wametengeneza madirisha mawili, la malalo ya Shekh Mufiid na Khawaja Nasrudini Tusi katika Atabatu Kadhimiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: