Muonekano wa furaha umeenea katika uwanja wa haram tukufu ya Abbasi, kufuatia kuwasili kwa Idi Ghadiir, korido za Atabatu Abbasiyya tukufu zimepambwa kwa mauwa yenye rangi nzuri za kupendeza, na katika kuta zake kumewekwa mabango yenye ujumbe wa kumtii kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), ikiwa kama sehemu ya kuonyesha furaha za wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kutokana na tukio hili tukufu la tangazo la kukamilika Dini tukufu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kumtangaza mtoto wa ammi yake na wasii wake Abu Hassan kiongozi wa waumini kua khalifa baada yake kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.
Kitengo cha utunzaji wa haram ambacho huwajibika kupamba haram katika kila tukio, kupitia kiongozi wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidiin Adnaan ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeupamba uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa zaidi ya mauwa elfu nne ya aina tofauti, yaliyo wekwa katika maeneo hamsini, ukitoa mauwa watakayo pewa watumishi na mazuwaru kesho wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya suku tukufu ya Ghadiir.
Akaongeza kua: “Kama inavyo julikana kwa kila tukio la kidini linalo husu watu wa nyumba ya Mtume (a.s) hua tunawasiliana na idara ya ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kushona vitambaa na mabango yanayo andikwa maneno ya kuonyesha utiifu kwa Ali bun Abu Twalib (a.s), vilevile hua tunapamba sehemu yatakapo fanyika maadhimisho kwa kuweka mauwa na mapambo mazuri zaidi”.