Mtandao wa kimataifa Alkafeel unawapongeza wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kufutia tukio la Idi Ghadiir…

Maoni katika picha
Hakika ameamrisha Mkuu Mtukufu (Mwenyezi Mungu) Mtume Muhammad afikishe ujumbe katika eneo la Ghadiir Khum… ilisikika sauti katika mbingi, kilele chake ilikua ni ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo iteremsha katika Qur’an (Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hautafanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake).

Litukuzwe jina lako ewe Ali umekua wasii kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mtume akasema katika siku ya hijja, taratibu! Mimi nimemtawaza Ali kuwa wasii, alizaliwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na atakua mzani wa viumbe, alizaliwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu amekua wasii wa kihashimiyya, leo hakuna upanga kama Dhulfiqaar wala hakuna kijana kama Murtadha Ali..

Kutokana na tukio hili tukufu, Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa pongezi za dhati kwa Mbashiri na Muonyaji Muhammad Almustwafa na mtoto wa ammi yake Ali Murtadha (a.s) na kwa Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Mahdi Almuntadhir (a.s) pamoja na Maraajii Dini watukufu na ulimwengu wa kiislamu wote kwa ujumla kutokana na Idi Ghadiir tukufu, Idi kubwa ya Mwenyezi Mungu na siku ya kukamilisha Neema na kukamilika Dini, na kutangazwa wilaya kwa kutawazwa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atujalie sisi na nyie kua miongoni mwa wanaoshikamana na uongozi wake, na atujaalie sehemu tukufu pamoja na kiongozi wa waumini (a.s), na aurejeshee umma wa kiislamu tukio hili ukiwa na amani kheri na baraka, hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: