Idi Ghadiir ni siku ya kukamilika Dini na kutimia Neema…

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu mtukufu alikamilisha Dini na akatimiza Neema kwa waumini pale alipo tangazwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) kua Khalifa, Wasii na Imamu baada ya Mtume (s.a.w.w) katika eneo la Ghadiir Khum, hakika siku hii ni sikukuu kubwa kwa sababu ni siku ya kukamilika Dini na kutimia Neema, Neema gani kubwa zaidi ya kukamilika Dini na kutimia Neema ya Mwenyezi Mungu, hakika yatupasa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Neema aliyo tupa katika siku hii tukufu.

Imepokewa kutoka kwa Abu Muayyad, Muwaffaq bun Ahmadi bun Muhammad Al-Makkiy Al-Khawarzamiy, aliye fariki mwaka wa 568 Hijiriyya, imepokewa kwa sanadi yake, kutoka kwa Abu Saidi Khudriy anasema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alipo waita watu kwa Ali (a.s) katika eneo la Ghadiir Khum na akaamrisha kutoa miba chini ya mti, ilikua siku wa Alkhamisi, akamwita Ali akamshika mkono wake na kuunyanyua hadi watu wakaona kwapa la Mtume (s.a.w.w) hakumuachia hadi ilipo telemka aya isemaya: (…Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni Neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini…).

Mtume (s.a.w.w) akasema: “Mwenyezi Mungu mkubwa kwa kukamilisha Dini na kutimiza Neema na kuridhia ujumbe wangu na uongozi wa Ali baada yangu”.

Imepokewa kutoka kwa Abu Qassim Ali bun Hassan bun Hibatu-Llahi Shafiiyyu anaye julikana kama ibun Asaakir, aliye fariki mwaka wa 571 Hijiriyya, kutoka kwa Abu Huraira anasema: Atakaye funga mwezi kumi na nane wa Dhulhijja ataandikiwa thawabu sawa na aliyefunga miezi sitini, nayo ni siku ya tukio la Ghadiir Khum, pindi Mtume (s.a.w.w) alipo shika mkono wa Ali na akasema: “Je! Mimi sio kiongozi wa waumini? Wakasema: Ndio! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ni kiongozi wetu). Akasema: Ambaye mimi ni kiongozi wake na Ali ni kiongozi wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: