Kwa picha: Makundi ya mazuwaru yanamiminika kwa aliyepewa kiapo cha utii -baiyya- (a.s) kwa ajili ya kuhuisha baiyya na utii kwa Wasii wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Makundi ya mazuwaru kutoka kila sehemu yanamiminika yakiwa yamebeba mauwa huku wakiimba kaswida za kuhuisha utii kwa Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) kama sehemu ya kuadhimisha siku ya Ghadiir na kuhuisha utiifu wao katika sikukuu hii kubwa.

Kufuatia ujio wa mamilioni ya mazuwaru vitengo na idara mbalimbali za Atabatu Alawiyya tukufu zikisaidiwa na mamia ya watu wakujitolea pamoja na vikundi vya Husseiniyya na wakazi wa mji mtukufu wa Najafu wamejipanga kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao.

Kumbuka kua sikukuu ya Idi Ghadiir ni sikukuu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu nayo ndiyo sikukuu kubwa zaidi kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hakuna Mtume yeyote ispokua alisherehekea siku hii na aliiheshimu, siku hii mbinguni inaitwa (siku ya ahadi iliyo ahidiwa) na hapa duniani inaitwa (siku ya ahadi iliyo tekelezwa na kundi lililo shuhudiwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: