Washerehekeaji wa Ghadiir baada ya kumaliza kula kiapo cha utii katika malalo ya mteule wa Ghadiir wanaelekea Karbala kuwapongeza watoto wake…

Maoni katika picha
Atabtu Alawiyya tukufu imeshuhudia makundi makubwa ya waumini walio kuja kuhuisha utiifu wao kwa Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na kuadhimisha kumbukumbu ya Idi Ghadiir kutoka ndani na nje ya Iraq, baada ya kumaliza kufanya ziara na kuomba dua wanaelekea Karbala ardhi ya shahada na utukufu, yaliko malalo ya watoto wake wawili Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na tukio hili tukufu la kukamilika Dini na kutimia Neema, pamoja na kusadifu kwake usiku mtukufu wa Ijumaa na kukutana matukufu mawili katika usiku mmoja, kila zama mkono wa Ali (a.s) hunyanyuliwa na Mtume (s.a.w.w), kila kizazi kinaungana na malaki katika bonde la Khum na kusikiliza wito wa milele usemao: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali ni kiongozi wake”.

Kama kawaida yake katika kila usiku wa Ijumaa Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua milango yake kuwapokea mazuwaru kutoka ndani ya mkoa wa Karbala na mikoa mingine pamoja na nchi za kiislamu na zisizo kua za kiislamu, haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imejaa mazuwaru kutoka maeneo mbalimbali, bila kujali ongezeko la joto la mazingira magumu ya safari.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia ratiba waliyo jiwekea kila usiku na mchana wa Ijumaa, wanafanya kila wawezalo katika kuwahudumia mazuwaru watukufu na kuwafanya waweze kutekeleza ibada ya ziara kwa amani na utulivu katika mazingira mazuri.

Kumbuka kua Idi Ghadiir ni sikukuu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu nayo ndiyo sikukuu kubwa zaidi kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hakuna Mtume yeyote ispokua alisherehekea siku hii na aliiheshimu, siku hii mbinguni inaitwa (siku ya ahadi iliyo ahidiwa) na hapa duniani inaitwa (siku ya ahadi iliyo tekelezwa na kundi lililo shuhudiwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: