Kufuatia Idi ya Ghadiir: Idara ya maelekezo ya kidini ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa zawadi kwa mubalighaat na wanafunzi wa Dini…

Maoni katika picha
Kufuatia sikukuu kubwa ya Mwenyezi Mungu Idi Ghadiir, Idara ya maelekezo ya kidini ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa iliyo iita (Ujumbe wa mbinguni unasambazwa kupitia midomo ya wanachuoni), kwa ajili ya kuwazawadia mubalighaat (500) pamoja na wanafunzi waliopata nafasi za kwanza katika shule za Dini za wasichana kwenye mkoa mtukufu wa Karbala, kutokana na juhudi zao kwenye uwanja wa tablighi au katika uwanja wa masomo.

Hafla hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa chini (sardabu) ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha likafuata tamko la ukaribisho lililo tolewa na mkuu wa idara Hajjat Ummu Hassan, mada zilizo wasilishwa zilihusu umuhimu wa siku ya Ghadiir, umuhimu wa elimu na umuhimu wa muda na namna ya kuutumia vizuri, semina za kielimu kwa namna yeyote zitakavyo kua, ziwe na muda mrefu au mfupi tutafaidika nazo iwapo tukijua namna ya kutumia muda na kuupangilia.

Hafla ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ilionyeshwa filamu isemayo: (Swada Marjaiyyah) vile vile palikua na mashindano ya somo la Fiqhi na Aqida, hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa wanafunzi wote kisha kwa wanafunzi walio fanya vizuri katika masomo yao na kwa wanafunzi walio hudhuria siku zote za ratiba ya hema za Skaut.

Kiongozi wa ofisi ya harakati katika idara ya maelekezo ya kidini amezungumzia kuhusu harakati hizi kua: “Hakika fikra ya kuanzisha shule za kidini ilikuja wakati Atabatu Abbasiyya ilipo wapokea waliohamishwa na kuvunjiwa nyumba zao, baada ya kutolewa fatwa tukufu ya jihadi ambayo Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria aliipa umuhimu mkubwa sana, ukaonekana umuhimu wa kupatikana malezi ya kidini, ndipo ikafunguliwa milango ya kuwapokea mabinti na kuwafundisha kusoma na kuanzika, na inatumika selibasi nzuri ya kimasomo inayo wawezesha kupata maarifa mbalimbali, kuchagua sekta ya mubalighaat (wahadhiri wa kike) kunatokana na mafanikio mabubwa ya wanafunzi katika masomo yao, pamoja na uwezo walio nao wanafunzi”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika mradi huu unamalengo mengi, miongoni mwa malengo yake ni kutengeneza mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi yatakao saidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, pamoja na kubainisha umuhimu wa kusomesha watoto wao hususan baada ya kutimliwa Daesh”.

Akamaliza kwa kutoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mzuri ulio rahisisha utendaji wote kwa ujumla.

Kumbuka kua vituo vya elimu na malezi vya Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kazi kwa kufuata utaratibu maalumu uliopangwa na Atabatu Abbasiyya, unao endana na maendeleo ya kielimu na kiutamaduni katika miji na vijiji, sambamba na maendeleo ya Dini katika jamii, baada ya kumaliza hatua ya kuwajenga wanafunzi kifikra sasa hivi imeanza kazi ya kusambaza walimu na mubalighaat katika shule za Dini, na hili ni jambo muhimu sana kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: