Vipengele muhimu katika khutuba ya swala ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (19 Dhulhijja 1439h) sawa na (31 Agosti 2018m) chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ilikua na vipengele muhimu vifuatavyo:

  • - Tuna haja kubwa ya elimu na utamaduni mzuri zaidi ya kula na kunywa.
  • - Vijana wa leo wapo katika hatari kubwa ya kiutamaduni na mmomonyoko wa maadili.
  • - Vijana wanatakiwa kutumia vizuri uwezo wao.
  • - Vijana ndio hazina ya taifa na jamii yawapasa wajuwe kinacho takiwa kwao.
  • - Elimu na utamaduni bora ni vitu muhimu sana yatakiwa kuzingatiwa.
  • - Tuangalie mipaka ya dunia inayo weza kumsaidia mwanadamu kurekebisha nafsi yake, inasikitisha kuwepo na mmomonyoko wa maadili na kuharibika utamaduni.
  • - Kuna sababu nyingi zinazo sababisha mmomonyoko wa maadili japo kua haifai Iraq kua hivi.
  • - Iraq sio taifa change katika utamaduni na wala sio taifa jipya katika maadili bali ni taifa kongwe.
  • - Tunataka kumbebesha kila mtu jukumu la kulinda utamaduni japo kidogo kuna baadhi ya mambo yanaweza kubakia katika uwanja wa ujinga.
  • - Kuna mvutano baina ya elimu na ujinga, elimu haikubali kukaa pamoja na ujinga na kinyume chake.
  • - Ukibishana na mjinga atakushinda.
  • - Kuna mjinga mwepesi (anaye jitambua) hutaka kujua na hapo mabishano hubadilika na kua mazungumzo yenye faida.
  • - Kila uwelewa unapo ongezeka maovu hupungua.
  • - Uovi hujikita kwa watu wajinga kila wanapo elimika uovu hupungua na kila elimu inapo ongezeka uovu huondoka.
  • - Ujinga hukaa sehemu isiyokua na elimu wala maadili mema.
  • - Baadhi ya wahitimu wa vyuo kwa masikitiko makubwa wakati mwingine hawajui hata kuandika majina yao au kuandika habari yeyote na kama akiandika itajaa makossa ya kilugha na ki-imla.
  • - Vijana wetu ndio mtaji inasikitisha kuwaona katika sehemu zisizo kua na faida yeyote na kuwa wavivu.
  • - Vijana msiwe wavivu nyie ndio walengwa wa fatwa, taifa, familia na jamii vinakuhitajini.
  • - Usiku upo kwa ajili ya kupumzika na mchana kufanya kazi muda ni angamizo la mwanadamu.
  • - Taifa, Marjaa na Familia wanahitaji kuona vijana wenye uwezo na utamaduni mzuri hivyo yawapasa vijana wachague elimu zitakazo komaza akili zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: