Chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki katika kongamano la kimataifa la udaktari, linalo fanyika katika mji wa Bazal huko Uswisi na kushiriki idadi kubwa ya vyuo vikuu vya kimataifa, wameshiriki kwa ajili ya kufahamu njia mpya za usomaji na usomeshaji wa kisasa katika vyuo vikuu vya udaktari, na kuboresha utendaji na uwezo wa wahitimu, na kutumia njia mpya katika utowaji wa mitihani, pamoja na kubadilishana uzowefu kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu ya udaktari.
Rais wa ugeni huo ambaye ni makamo rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Jaasim Ibrahimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ushiriki wetu katika kongamano hili la kielimu unatokana na imani yao kwa chuo pamoja na namna kinavyo yapa umuhimu makongamano ya aina hii na kuwasiliana kwake na wakufunzi wa vyuo vikuu wa masomo tofauti, kwa ajili ya kuboresha selebasi, pia ushiriki huu ni moja ya njia ya kufahamu uzowefu wa wengine katika sekta ya ufundishaji wa udaktari na kutambua maendeleo yaliyopo katika sekta hii, jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uhusiano wa wakufunzi na uwezo wa walimu katika kutambua mbinu za kimkakati zinazo tumika katika ufundishaji”.
Akabainisha kua: “Hakika kushiriki katika kongamano hili ni sehemu ya kuongeza elimu katika kitivo cha udaktari na kutambua maendeleo ya juu kabisa yaliyo fikiwa katika udaktari wa sasa duniani, na kuboresha misingi ya utumiaji wa selibasi hizo katika ratiba za usomeshaji”.
Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa makongamano ya kimataifa na linahudhuriwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu kutoka katika nchi tofauti, kwa kua kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed kinatumia selibasi ya udaktari mpya inayo tegemewa na chuo cha Leestar cha Uingereza na ambayo ndio selebasi ya kisasa zaidi duniani, ikawa ni muhimu tuwepo katika kongamano hili, lenye mada nyingi pamoja na mikakati ya utendaji wa kazi na mijadala mbalimbali ya kitaalamu, zaidi ulikua ni mjadala wa mbinu za ufundishaji wa Udaktari na selebasi mpya kwenye vyuo vya udaktari duniani.