Wahitimu wa Skaut zaidi ya (500): Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yahitimisha mafunzo ya kujenga uwezo hatua ya pili…

Maoni katika picha
Kutokana na hafla zinazo fanywa na waumini sehemu mbalimbali za Idi Ghadiir, Jumuiya ya Skaut Alkafeel ambayo ipo chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha mafunzo ya hatua ya pili, yaliyo andaliwa kwa ngazi ya (Ashbaal, Alkashaafah na Aljawaal) kwa vijana wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nane, kila ngazi ilikua na masomo maalumu yanayo endana na umri wao, yanayo lenga kujenga vijana wanaojitambua na wenye maadili mema kielimu na kiutamaduni, wenye elimu bora ya dini itokanayo na turathi za Ahlulbait (a.s), na kusaidia katika kubaini vipaji na uwezo walio nao na kuuendeleza kinadhariyya na kivitendo.

Hafla ya kuhitimisha masomo hayo imefanyika katika jengo la Sheikh Kuleini (r.a) na kushiriki zaidi wa wahitimu (500) wa Skaut, pamoja na wanaskaut wengine kutoka mikoani na ujumbe rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi na Surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na kusikiliza wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu, yalifuata maonyesho ya Skaut.

Kisha ukafuata ujumbe kutoka katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na rais wa kitengo hicho Sayyid Liith Mussawi, alianza kwa kutoa pongezi za Idi Ghadiir kisha akabainisha kua: “Nawapongeza kwa kuhitimu hatua hii ya kujenga uwezo iliyo andaliwa na ndugu zetu wa idara ya watoto na makuzi, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ajalie mafunzo haya yawe na faida kwa watoto wetu walio shiriki katika program hii”.

Ukafuata ujumbe kutoka katika jumuiya ya Skaut ulio wasilishwa na kiongozi wa maendeleo katika jumuiya hiyo Dokta Zamani Alkinani, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tunapo funga ratiba hii ya kujenga uwezo, baada ya kutoa shukrani na pongezi kwa kila aliye changia mafanikio haya, yatupasa kutambulisha japo kwa ufupi mbele ya wageni wetu sura ya mafunzo haya na malengo yake pamoja na dira yetu, kwa nini tumetoa mafunzo haya? Kitugani kilicho tusukuma hadi tukaandaa mafunzo haya? Tunapanga, tunafanya, tunasonga mbele, hatua ya pili ya mafunzo haya yalikua na vipindi vya mihadhara, pamoja na warsha na masomo mbalimbali chini ya walimu wazowefu na wabobezi wa fani mbalimbali za Dini, Aqida na tamaduni, kutokana na kuhisi kwetu majukumu ndio kuliko tufanya tuandae masomo haya, ikiwa ni pamoja na kupambana na upotoshaji wa vyombo vya habari, pamoja na michezo ya kielektronik isiyo faa na baadhi ya mitandao ya kijamii ya video, na kubainisha mema yake na mabaya yake yanayo haribu familia za kiislamu, tulijikita katika kubainisha mambo yanayo haribu familia za wairaq na jamii ya kiislamu kwa ujumla”.

Akaongeza kua: “Mafunzo ya Skaut na michezo pamoja na vitu vingine vilifungamana na ratiba ya kuwajengea uwezo, lengo kuu likiwa ni kuwaandaa vijana kifikra, kiutamaduni na kijamii, katika kuyafanya haya tunatekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani, vijana wetu wa leo wanatuangalia sisi, lazima tuwe na mikakati imara ya kupambana katika vita ya kiutamaduni na kifikra, hatuwezi kukubali waharibike, watoto wenu ni amana kwetu”.

Hafla ilipambwa na maonyesho ya video iliyokua na mambo kadhaa yaliyo fanyika katika mafunzo haya pamoja na baadhi za harakati zinazo fanywa na jumuiya, hafla ikahitimishwa kwa kugawa midani na vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya Skaut na wale walio saidia kufanikisha mafunzo haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: