Maandalizi ya kumbukumbu ya maombolezo ya Ashura: kitengo cha mawakibu na maadhimisho chafanya mkutano na kusisitiza kufuata maelekezo na kulinda mali za umma…

Maoni katika picha
Jirani na malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) kitengo cha mawakibu, maadhimisho na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya alasiri ya Juma Mosi (20 Dhulhijja 1439h) sawa na (1 Septemba 2018m) kimefanya mkutano wa kujadiliana kuhusu maombolezo ya Ashura, wamejadili swala la mpangilio, utowaji wa huduma na usalama, mkutano huo wamefanyia katika ukumbi wa Khatamul Anbiyaa (s.a.w.w) ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu mkoani Karbala.

Mkutano ulifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ulio wasilishwa na rais wa kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, akabainisha kua: “Hakika wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wana pande mbili, wana Idi Ghadiir na Ashura ya Imamu Hussein (a.s), kila mwaka huwa tunafanya mkutano huu wa kujadiliana na kushauriana tukiwa pamoja na wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Karbala, pia tukiwa pamoja na wawakilishi wa serikali ya Karbala na kujadiliana mambo ya kuimarisha usalama na kuboresha utowaji wa huduma, kwa ajili ya kuhakikisha maombolezo haya yanafanyika kwa amani na utulivu na katika mazingira bora zaidi, jambo ambalo haliwezi kufikiwa kama hakutakuwa na ushirikiano, katika mkutano huu huwasilishwa mambo yote yanayo husiana na maombolezo ya Ashura katika mji mtukufu wa Karbala, mji wa shahada na utukifu, hakika kitengo cha maadhimisho ni chenu na kinatokana na nyie, kwa kuonganisha juhudi zetu tunaweza kufanya maomboleza haya katika mazingira mazuri, yakaonekana kweli ni maombolezo yenye misingi ya harakati ya Imamu Hussein (a.s)”.

Ukafuata ujumbe kutoka katika kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo hicho Bwana Maazin Alwazni ambaye alisisitiza kua: “Ni muhimu kufuata maelekezo yatakayo saidia kufanyika maombolezo na utowaji bora wa huduma pamoja na mambo mengine, watumishi wa mawakibu wanatakiwa kutafsiri misingi ya harakati ya Imamu Hussein (a.s) katika kuhuisha kumbukumbu ya kifo chake, tunatarajia wafuate sheria na kushikamana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu katika kuomboleza na wasiharibu mali za umma”.

Baada ya hapo ukafunguliwa mlango wa kujadiliana wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya pamoja na wawakilishi wa vitengo vya huduma na usalama vya serikali ya mkoa, ambao waliwasilisha mikakati yao katika utekelezaji wa maomboleza haya, ambapo walisikilizwa na wakasherehesha baadhi ya vipengele vilivyo hitaji maelezo zaidi, pamoja na kupata maoni yaliyo lenga kuboresha utekelezaji wa maadhimisho haya na kujiepusha na kila aina ya upungufu na kasoro.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: