Sherehe mbalimba za Ghadiir zafanyika chini ya usimamizi wa kitengo cha eneo la katika ya haram mbili tukufu…

Maoni katika picha
Uhuishaji wa sherehe za kumbukumbu ya siku ya ahadi iliyo ahidiwa, na agizo lililotekelezwa na kundi lililo shuhudiwa, siku ya kukamishwa Dini na kutimizwa Neema na uteuzi wa Mwenyezi Mungu, siku ya Ghadiir Idi ya Wilaya na Idi wa Uimamu mkuu, sikukuu ya Mwenyezi Mungu kuwakamilishia waumini Dini na Neema yake kwa kutangazwa Amirul Mu-uminina Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa ni Walii wa walimwengu na khalifa wa Mtume (s.a.w.w), kwa nyoyo zenye furaha na imani kubwa, kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimesimamia matukio mbalimbali ya sherehe yaliyo endelea kufanyika kwa siku kadhaa, na kimeandaa mazingira ya kufanikisha sherehe hizo na kuhuisha utiifu kwa bwana wa mawasii (a.s) katika eneo tukufu zaidi duniani, eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Miongoni mwa harakati za kusherehekea zinazo fanyika ni mahafali za usomaji wa mashairi ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ambazo washairi mahiri wa maadhimisho ya Husseiniyya wanashiriki kwa kuimba kaswida za kumsifu na kuonyesha mapenzi kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) pamoja na watoto wake Maimamu watakasifu (a.s), zikiwemo kaswida za kuonyesha mapenzi kwa taifa la Iraq na vionjo vya kijamii vinavyo furahisha nyoyo za wasikilizaji.

Kwa upande mwingine chini ya kauli mbiu isemayo (kwa Sanaa na utamaduni tunasherehekea) taasisi ya Badru Munirah ya misaada na maendeleo, imefanya maonyesho ya mabango yenye picha za kuchorwa za Baiyya ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) katika eneo tukufu la Ghadiir Khum, maonyesho hayo yamefanyika katika moja ya sehemu zenye paa za eneo ya katikati ya haram mbili tukufu, sambamba na kufanya kongamano la usomaji wa mashairi ambalo wameshiriki washairi wakubwa kama vile Ali Najjaari Ka’abiy na Husseini Nasoro Karbalai.

Kumbuka kua harakati hizi zinafanyika chini ya ratiba maalumu ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu ya kufanya mahafali na majlisi za matukio ya kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu watakasifu (a.s) na maswahaba wakubwa (r.a).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: