Kati ya nchi (32): Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yapanda jukwaani na kuhutubia kongamano la kimataifa la themanini na nne la maktaba na taaluma nchini Malezia…

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imepanda jukwaani na kuhutubia kongamano la kimataifa la themanini na nne la maktaba na taaluma, linalo andaliwa na umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba (Ifla) katika mji mkuu wa Malezia, chini ya kauli mbiu isemayo: (Kubadilisha mwenendo wa maktaba ni njia ya kubadilisha jamii), linalo angazia nafasi ya athari za maktaba katika kubadilisha jamii na umma na kuleta maendeleo, ambalo limehudhuriwa na zaidi ya nchi (110) zilizo wakiliswa na washiriki zaidi ya (3500) wawakilishi wa nchi (32) ndio walio teuliwa kuzungumza, hii ni mara ya kwanza Iraq kuwakilishwa katika kongamano hili na imekua nchi ya pili katika inchi za kiarabu pamoja na Qatar.

Mwakilishi wa Maktaba Ustadh Hussein Aadil amezungumza kwa lugha ya kiengereza sambamba na kutumia video, mada inayo husu (Maktaba za Iraq baada ya Daesh), alielezea maktaba kuu ya chuo kikuu cha Mosul na majanga yaliyo ikumba ya kuvunjwa na kuchomwa na magaidi wa Daesh, na mchango wa maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuifufua maktaba ya chuo kikuu cha Mosul na kutafuta ufumbuzi wa kuzuwiya matukio ya aina hiyo kwa kuanzisha mradi wa kitaifa wa kulinda turathi za kielimu za Iraq, mradi ambao ulikuja na mbinu ya kuhifadhi kumbukumbu za kielimu na kiutamaduni kwa kuchukua vitabu, barua (ujumbe) wa vyuo vikuu vya zamani vya Iraq na kuhifadhiwa kiteknolojia na namna ya utekelezaji wa mradi huo.

Wakati anazungumza Ustadh Hussein alisikilizwa kwa makini huku ukumbi ukiwa kimya kabisa, na baada ya kumaliza alishangiliwa kwa nguvu sana, kwa sababu wahudhuriaji wengi walikua hawajui mbinu alizo kua anazielezea na wengine waliona kwenye vyombo vya habari tu, kwa hiyo ilikuwa fursa muhimu kwao kupata maelezo moja kwa moja kutoka kwa mtaalamu, kisha waliuliza maswali kwa wingi sana akasimama na kujibu sambamba na kusherehesha zaidi pale palipo hitaji kushereheshwa.

Kumbuka kua kongamano la Ifla ambalo huwa na mada nyingi, linahudhuriwa na watu waliobobea katika sekta ya maktaba kutoka kila sehemu ya dunia kila mwaka, kongamano la mwaka huu limeandaliwa na umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba (Ifla), pamoja na jumuiya na maktaba kuu ya Malezia, chini ya ufadhili wa wizara ya utalii na utamaduni ya Malezia na ofisi ya maonyesho na makongamano ya Malezia, ushiriki wa maktaba na Daru Maktutwaat ya Atabatu Abbasiyya ni wa mara ya kwanza katika ngazi ya Ataba tukufu na wa mara ya kwanza katika ngazi ya taifa la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: