Shahidi wa Aqida na utukufu Maitham Tammaar (r.a)…

Maoni katika picha
Anaitwa Maitham bun Yahya Tammaar, alizaliwa katika mji wa Nahrawaan Iraq, na alikua mtumwa wa mwanamke wa bani Asadi, kisha akasilimu na kununuliwa na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na kuachwa huru, akawa karibu sana na Imamu Ali (a.s) kama vile mtu na kivuli chake, akawa anatembea pamoja naye kama vile mtoto wa mbuzi na mama yake, akajifunza elimu na maarifa zaidi ya watu wengine walivyo jifunza kutoka kwa Imamu (a.s).

Yatosha kujua utukufu wake pale alipo muambia ibun Abbasi: Niulize chochote katika tafsiri ya Qur’an hakika mimi nilisoma uteremshwaji wake kutoka kwa kiongozi wa waumini (a.s) akanifundisha na ta-awili yake, ibun Abbasi hakukanusha kauli hiyo, alisimama na kuchukua kalamu na wino ili aandike atakayo ambiwa na Maitham. Maitham alikua anafanya kazi ya kuuza tende, alikua na duka la tende, ndio akapewa jina la Tammaar (muuza tende), alikua anafundisha fadhila na utukufu wa Imamu Ali kwa njia maalumu pamoja na fadhila za Ahlulbait (a.s), na alikua anafichua uwongo wa bani Umayya hususan Muawiya na wafuasi wake, Maitham aliendelea kuelezea utukufu wa bani Hashim.

Ibun Ziyadi aliamuru akamatwe na kuletwa mbele yake, akamuambia: Jitenge na Ali (a.s) na umtawalishe Othmaan ukikataa nitakata mikono yako na miguu yako na nitakusulubu, Maitham (r.a) akakataa, akaendelea kutaja utukufu na elimu ya Imamu Ali (a.s), mtoto wa mama muovu Ubaidullahi bun Ziyadi akaamrisha akatwe mikono yake na miguu yake na akamsulubu kwenye ubao, alipo pandishwa juu ya ubao akasema kwa sauti ya juu: Enyi watu, anaye taka kusikia hadithi maknuun kutoka kwa Ali bun Abu Twalib kabla ya kuuawa kwangu, wallahi takuambieni mambo yatakayo tokea hadi siku ya kiyama na fitna zitakazo tokea.

Akaanza kuelezea watu utukufu wa Ali bun Abu Twalib (a.s) na utukufu wa bani Hashim na miujiza yao, na akaelezea maovu ya bani Umayya akiwa anasulubiwa juu ya mbao, ibun Ziyadi akaambiwa: Hakika mja huyu amekufedhehesheni, akasema: Mgigeni mawe, wakaanza kumpiga mawe baada ya kumchoma mkuki, alikua ni mtu wa kwanza katika uislamu aliye pigwa mawe huku anaongea, baada ya pua na mdomo kujaa damu, maluuni ibun Ziyadi akaamrisha akatwe ulimi wake, wakakata ulimi wake, ndevu zake zikajaa damu, kisha maluuni akamchoma mkuki wa chini ya mbavu ukammaliza, akasoma takbira na roho yake tukufu ikatoka.

Maitham Tammaar (r.a) alisulubiwa na kuuawa siku ya juma pili mwezi ishirini Dhulhijja na akazikwa katika mji wa Kufa, kaburi lake lipo hadi leo na hutembelewa na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), sehemu alipo zikwa ni karibu na Masjid Kufa upande wa kusini magharibi kushoto kwa mtu anaye kwenda Najafu kutoka Kufa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: