Katika watu (35) walio shiriki: Msomaji na muadhini wa Atabatu Abbasiyya tukufu awa mshindi wa kwanza katika shindano la Ghadiir la kitaifa la kuadhini…

Maoni katika picha
Msomaji na muadhini wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Haidari Jalukhaan Mussawi amekuwa mshindi wa kwanza katika shindano la Ghadiir na kitaifa la kuadhini, lililo simamiwa na kitengo cha dini na idara ya Darul Qur’an chini ya uongozi mkuu wa Masjid Kufa na mazaru zinazo fungamana nayo, katika jumla ya watu (35) walio shiriki shindano hilo kutoka katika Ataba mbalimbali na taasisi za Qur’an.

Shindano hili ni sehemu ya kusherehekea Idi Ghadiir, lilikua na jumla ya washiriki (35) ambapo kila mkoa umewakilishwa na washiriki wawili walio chaguliwa na taasisi na vikundi vya usomaji wa Qur’an katika mikoa hiyo, ispokua mkoa wa Basra na Bagdadi imetuma washiriki (4) kila mkoa, pamoja na kushiriki waadhini wa Ataba mbalimbali na kituo cha taifa cha maarifa ya Qur’an na kamati ya Hashdi Sha’abi kwa kuleta wawakilishi wawili kila mmoja.

Shindano hilo lilisimamiwa na kamati ya majaji watatu mahiri, walio bobea katika hukumu za tajwidi, naghma na sauti, Sayyid Haidari Jalukhaan akafanikiwa kupata max (alama) zilizo muwezesha kuwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili alikua ni Sayyid Hussein Ma’allahi Abdul-Aali kutoka mji mkuu wa Bagdadi, naye Sayyid Ridha Muhammad Mahdi kutoka Bagdadi akapata nafasi ya tatu katika mashindano haya.

Kumbuka kua wasomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamesha shiriki mara nyingi mashindano ya kimataifa na kitaifa, mengi kati ya hayo walipata zawadi na nafasi za juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: