Majemedari wa shahada na watumishi wema: Miongoni mwa visa vya mashahidi walio sababisha ushindi dhidi ya Daesh (Shahidi Sayyid Wasaam Sharifu Mussawi)…

Maoni katika picha
Ni desturi ya watu kujifaharisha kwa mashujaa wao watukufu ambao hubakizwa na historia, kwa kusimulia visa vyao kwa vizazi vijavyo na kuandika vitabu vinavyo wazungumzia, na kuwafanya kuwa mfano wa kuigwa, tunapo zungumzia mashujaa wema; acha tuenzi msimamo wa jihadi na ushujaa uliotunzwa na historia, tunakiri ushujaa wa kijana wa kiiraq aliye fuata nyayo za ushujaa wa babu zake katika mapambano ya ishirini na maandamano ya Shaabaniyya matukufu.

Kutokana na kuendeleza utukufu wao Shahidi wetu aliweza kuendeleza utukufu huo, Sayyid Wisaam Sharifu Mussawi (r.a) alizaliwa katika familia ambayo zawadi yao na nasaba yao ni kuwapenda Ahlulbait (a.s), alikua mwingi wa kuhudhuria vikao vya maombolezo ya Imamu Hussein katika mkoa wa Basra, mwaka (2003) alifanya kazi katika ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani, kisha alijitolea kulinda taasisi za serikali mwanzoni mwa uvamizi wa Marekani ikiwa ni pamoja na hospitali ya Hussein (a.s) mjini Karbala, mwaka (2014m) alifanya kazi katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kwa ajili ya kupata riziki yake, kwa kua alikua kiongozi muadilifu alishiriki mara nyingi kutatua migogoro ya kijamii na kikabila, alikua na uhusiano mzuri na viongozi wa makabila ya Iraq kuanzia katikati ya nchi hadi kusini.

Aliishi katika mji wa Hussein (a.s) Karbala tukufu, alikua mtu mwenye roho nzuri na tabia njema, kila aliye mtambua alisimulia ukarimu alio kuwa nao wakati wa uhai wake, alisoma katika hauza (shule) za Dini tukufu na alishikamana na mafundisho ya Dini pamoja na maelekezo ya Maimamu watakasifu (a.s), baada ya fatwa tukufu ya jihati ya kujilinda, alijiunga na wapiganaji wa kujitolea dhidi ya magaidi ya Daesh, akawa kamanda katika moja ya vikosi vya Abbasi (a.s) tangu mwanzo wa kuanzishwa kwake, alishirika sehemu nyingi za mapigano na kutoa somo kali kwa Daesh kutokana na ushujaa alio kuwa nao na moyo wa kujitolea, hadi walipo amua kusafisha kitongoji cha (Sayyid Ghuraib) katika mji wa Balad (ambao upo magharibi ya wilaya ya Balad) ndipo alipo viziwa na mlenga shabaha wa maadui akafa shahidi akiwa amelowa damu za utukufu wakati wa adhana ya Adhuhuri, baada ya kumaliza kuimba mimbo ya wilaya na hamasa akiwa mstari wa mbele wa wapiganaji, mwili wake ulibakia katika uwanja wa vita zaidi ya siku moja kutokana na ugumu wa kuufikia kufuatia mapigano makali yaliyo kua yanaendelea eneo hilo.

Utukufu na kuenziwa ni kwa watu kama wewe ewe jemedari mtukufu, kukuenzi ni jambo kubwa, umeacha historia njema, umepigana jihadi bora katika ardhi takatifu, umepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu hadi ukauawa kishahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: