Mkakati wa taasisi ya (IDA) chini ya anuani isemayo: Kongamano la tatu la wataalamu wa Iraq katika chuo kikuu cha Al-Ameed…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtazamo wa pamoja, ufundishaji endelevu… ni msingi wa mafanikio), wataalamu wa kuendeleza nafsi kwa kushirikiana na chuo cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kongamano ndani ya ukumbi wake mkuu la kuweka mikakati ya taasisi za Iraq (IDA), na kuhudhuriwa na viongozi wa kisekula na kitamaduni kutoka nje na ndani ya mkoa wa Karbala.

Kongamano hilo lilikua na vipengele vingi vya kijamii na mihadhara ya kisekula inayo lenga kukuza kiwango cha sekula na kuongeza uwezo wa kipaji kwa mtu mmoja mmoja na kuongeza ufanisi, pamoja na kupevusha fikra na mbinu za kielimu vitu ambavyo vinauhusiano mkubwa na utendaji wa kazi.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Al-Ameed kilikua kimesha fungua milango ya mawasiliano na kusaidiana na taasisi mbalimbali za kijamii na kielimu kwa kufanya nadwa na warsha za kielimu za pamoja, zinazo lenga kuboresha utendaji wa taasisi za kijamii katika sekta mbalimbali, kwa namna ambayo matokeo yake yataonekana moja kwa moja katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: