Kamati ya msaada wa kimkakati na kimaanawiyya chini ya kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, haijaishia kutoa misaada ya vitu na kimkakati peke yake kwa wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abi, bali kuna majukumu mengine ambayo ni sehemu ya pili ya majukumu yake ya kusaidia inayo wapa moyo na msimamo zaidi wapiganaji.
Ugeni maalumu wa kamati hiyo ukiongozwa na kiongozi wao Shekh Haidari Aaridhi umeshiriki katika mahafali ya kuhitimu askari watembea kwa miguu wa Hashdi Sha’abi walio pata mafunzo katika chuo cha kijeshi Askariyyaini (a.s) kilichopo wilaya ya Balad, Shekh Aaridhi alizungumza katika mahafali hayo, aliwapongeza wapiganaji kutokana na moyo wa kupigana walio nao, akawahimiza kufaidika na mafunzo waliyo pata, kwani mafunzo yana nafasi kubwa ya kuongeza uwezo wa mpiganaji na uzowefu wa kutumia siraha mbalimbali katika uwanja wa vita, na kuongeza kiwango cha utendaji wa pamoja kama tim moja katika kila hatua ya vita ambalo ni jambo la lazima kwa kila askari.
Mwisho mwa hafla, wahitimu walikongwa nyoyo kwa kupewa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na zawadi ya thamani.
Wahitimu walishukuru sana jambo hili lililofanywa na kamati, wakasema zawadi hizi ni kilele cha utukufu kwao, kwani inatoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).