Mwezi ishirini na tatu Dhulhijja ni kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Ibrahim na Muhammad mayatima wawili ambao ni watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s)…

Maoni katika picha
Watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s) walikua kama baba yao, walionyesha ushujaa wa hali ya juu mbele ya waovu na madhalimu, hili sio geni kwani wanatokana na kizazi kitakatifu kilicho ridhiwa, kuuawa kwao ni kawaida na utukufu wao mbele ya Mwenyezi Mungu ni Shahada.

Shekh Swaduuq (r.a) ametaja kisa cha mashahidi wawili hawa Muhammad na Ibrahim, anasema: Watoto wawili hao walitekwa kutoka katika watu wa Imamu Hussein (a.s), wakapelekwa kwa Ibun Ziyadi, akawakabidhi kwa mtu (bwana jela), mtu huyo akawabusu na kuwaomba samahani kwa waliyo fanyiwa kutokana na heshima waliyo nayo mbele ya Mtume (s.a.w.w), kisha akawaambia: Ukiingia usiku nitakufungulieni mlango wa jela, mwende kokote mnako taka, ulipo ingia usiku akawatoa jela na akawaambia: tembeeni usiku, ukifika mchana mjifiche muendelee kufanya hivyo hadi Mwenyezi Mungu atakapo kufanyieni wepesi.

Wakakimbia watoto hao, ulipo fika usiku mwingi wakamkuta bibi amesimama mlangoni kwake anamsubiri kijana wake, wakajitambulisha kwa bibi huyo, wakamuambia wao ni wageni na wanatokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w) na hawajui wanako elekea, wakamuomba awape hifadhi usiku huo.

Bibi akawakaribisha ndani, akawapa chakula na maji, wakala na kunywa, wakalala wakiwa wanatarajia amani, wakalala huku wamekumbatiana, usiku huo huo kijana wa bibi akarudi akiwa amechoka na kazi ya kuwatafuta watoto hao, akamuelezea bibi kisa cha kutoroka watoto wawili katika jela ya Ibun Ziyadi, na kwamba amewaambia askari wake yeyote atakaye leta vichwa vya watoto hao atapewa dirham eflu moja.

Bibi akamtahadharisha na adhabu kali ya Mwenyezi Mungu akamuambia; jambo hilo ni kutafuta ugomvi na babu yao Muhammad (s.a.w.w), jambo hilo halina faida kwake duniani wa akhera, kijana akawa na wasiwasi kutokana na mawaidha hayo, akahisi bibi huyo atakua amewafisha watoto hoa, lakini bibi hakumuambia kitu, alimficha uwepo wa watoto hao katika nyumba yake, kijana yule akaanza kuwatafuta ndani ya nyumba hiyo hadi akawaona wakiwa wamelala, akawauliza: nyie ni wakina nani? Wakamuambia: Tukikwambia ukweli unatuthibitishia usalama? Akajibu: ndio. Akawathibitishia usalama mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akamfanya Mwenyezi Mungu ndio shahidi na wakutegemewa, akawasimamisha (wakabaki wamesimama hadi asubuhi).

Ilipo fika asubuhi akamuagiza mfanya kazi wake (alikua ni mtu mweusi) aende nao pembeni ya mto Furat awachinje na ampelekee vichwa vyao, walipo chukuliwa na kijana huyo wakamuambia: Ewe mtu mweusi, weusi wako unafanana sana na Bilali Muadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi unataka kutuua wakati sisi tunatokana na kizazi cha Mtume wako?! Wakamuhadithia kisa chao na jinsi walivyo fungwa na mambo yaliyo tokea hadi bibi akawakaribisha katika nyumba yake.

Kijana mweusi akaingiwa na huruma na akawaomba samahani, akatupa upanga wake na akajitosa mtoni akaogelea hadi upande wa pili wa mto, bosi wake akamwita kwa sauti ya juu: Umeniasi? Akamjibu: Mimi nitakutii kama hautamuasi Mwenyezi Mungu, ukimuasi Mwenyezi Mungu mimi nitakua mbali na wewe.

Mtu huyo hakuwaidhika wala roho yake haikuingia huruma, alimwita mwanaye akamuambia: Hakika Dunia imekukusanyia halali na haram, na Dunia inatafutwa wauwe vijana (watoto) wawili uniletee vichwa vyao nipeleke kwa Ibun Ziyadi, mwanaye alipo wafuata watoto hao wakamuambia: Ewe kijana hauhofii ujana wako kuuingiza katika moto wa jahanamu sisi tunatokana na kizazi cha Mtume Muhammad. Kijana akaingiwa na huruma akafanya kama alivyo fanya mtumwa.

Yule mtu akasema: Nitawachinja mimi mwenyewe, watoto wakamuambia: Kama unataka mali tupeleke sokoni ukatuuze na hautakua miongoni mwa wagonvi wa Muhammad kwa sababu ya kizazi chake, kama hilo ni zito, tupeleke kwa Ibun Ziyadi tukapate rai yake, jamaa akakataa, wakamuambia: Hauogopi heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (kwa kuua watu wa kizazi chake), akakanusha ukaribu wao kwa Mtume (s.a.w.w), pamoja na udogo wa umri wao haukusaidia kulainisha moyo wake.

Wakamuomba awape mda wa kuswali, akawaambia: swalini kama swala itakusaidieni, walipo maliza kuswali wakanyanyua mikono yao juu wakasema: Ewe uliye hai ewe mpole, ewe hakimu wa mahakimu hukumu baina yetu na baina yake kwa haki (Yaa Hayyu yaa Haliim, yaa Ahkamal Haakimiin uhkum bainanaa wa bainahu bilhaqi).

Akamshika mtoto mkubwa akamchinja, yule mdogo akalowa damu za kaka yake, akasema: Hivi ndinyo nitakavyo kutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu nikiwa nimelowa damu za kaka yangu, akamchinja na mdogo na kukata vichwa vyoa kisha miili yao akaitupa katika mto wa Furat, akapeleka vichwa kwa Ibun Ziyadi na akamsimulia mambo aliyo shuhudia kwa watoto hao.

Mwenyezi Mungu mtukufu alikubali dua za watoto wale, akamnyima Dunia na Akhera, Ibun Ziyadi akamuambia: Hakika hakimu wa mahakimu (Ahkamal haakimiin) amehukumu uuliwe, akachukuliwa hadi sehemu alipo waulia wale watoto akakatwa kichwa chake na kikatungikwa juu ya mkuki wakaamrishwa watoto wakipige mawe huku wanasema: Huyu ni muuwaji wa familia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kaburi zao tukufu (watoto hao) zipo umbali wa kilometa tatu mashariki ya wilaya ya Musayyib upande wa mashariki wa mto Furat, kwa sasa eneo hilo kiserikali lipo chini ya mji wa Hilla katikati ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: