Maandalizi ya kuchagua watakao shiriki katika mashindano ya kimataifa: Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake yaandaa mashindano ya kuhifadhi Qur’an…

Maoni katika picha
Kwaa ajili ya kujiandaa na kuwanoa mahafidhi wa Qur’an pamoja na kuchagua watakao shiriki katika mashindano ya kimataifa, Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mashindano ya kuhifadhi Qur’an na kuyapa jina la: (Alfurqaanu kuhifahi Qur’an tukufu maandalizi ya pili), na kushiriki mahafidhu wa Qur’an kutoka vituo na taasisi tofauti za Qur’an katika mkoa wa Najafu Ashrafu pamoja na wanafunzi wa Maahadi ya wasichana, chini ya usimamizi wa kamati ya majaji walio bobea na wanaokidhi vigezo vya kimataifa vinavyo tumika katika mashindano ya aina hiyo.

Mahafidhi wamewekwa katika vikundi, kazi ya kuwatahini imefanyika kwa muda wa siku tatu, chini ya mazingira mazuri yaliyo jaa nuru ya Qur’an itokanayo na visomo vizuri vya sauti nzuri zilizo jaa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, wamehifadhi viwango tofauti kuanzia juzuu tatu hadi Qur’an nzima, wamekuja kushiriki katika mashindano haya mahafidhi wa aina tofauti.

Kumbuka kua lengo la kuanziahwa kwa Maahadi ya Qur’an tayi la wanawake lililopo katika mkoa wa Najafu mtaa wa Karaamah ni kusambaza elimu ya Dini kwa wanawake ikiwemo elimu hii tukufu ya “Maarifa ya Qur’an” na kuchangia katika kuandaa kizazi cha wanawake wanao jitambua watakao weza kuhuisha sunna na kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’an tukufu, pia inakusudia kukifundisha kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na kuifanyia kazi Qur’an tukufu kwa vitendo na kauli pamoja na kupambika na tabia njema, na kulingania chini ya misingi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume na Aali zake watakatifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: