Mawakibu na watu wa Karbala wameanza kujiandaa kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu za Ashura…

Maoni katika picha
Watu wa Karbala wameanza kujiandaa kuupokea mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam, kama kawaida maandalizi haya yameanza baada ya kusherekekea Idi ya Ghadiir chini ya usimamizi na ulinzi mkali, maandalizi hayo yanasambaa kwa haraka katika mji wa Karbala.

Kutokana na kukaribia mwezi wa huzuni ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba zake, yameanza maandalizi ya kuhuisha maombolezo hayo katika sekta zote za utowaji wa huduma na maombolezo, mapambo meusi yameanza kujaa katika mji wa shahada kidogo kidogo, mawakibu nyingi na vikundi vya Husseiniyya wameanza kujenga mabanda na mahema kwa ajili ya kujiandaa na utowaji wa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.

Maandalizi haya yalitanguliwa na vikao kadhaa baina ya watu wenye mawakibu na kamati za maombolezo za watu wa Karbala, pamoja na kikao cha pamoja kilicho husisha viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na kitengo cha maadhimisho cha Ataba mbili tukufu pamoja na wawakilishi wa serikali wa kamati ya amani na huduma, ambacho walikubaliana mambo mengi yatakayo saidia kufanikisha maombolezo haya na kuyafanya yaendane na sura halisi ya harakati ya Imamu Hussein (a.s).

Barabara na mitaa ya mji mtukufu wa Karbala hasa katika eneo linalo zunguka malalo mawili matukufu linashuhudia ujenzi kila siku wa mawakibu na sehemu za kufanyia majlis za maombolezo na kugawa chakula pamoja na huduma zingine, miongoni mwa mambo muhimu yanayo fanywa na watu wa Karbala wakati wa maombolezo haya ambayo huzingatiwa kua ni urithi wa Ashura walio nao watu wa Karbala.

Watumishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya wanakamilisha maandalizi yote kwa ajili ya kutowa huduma kwa mazuwaru ambazo mara nyingi haziishii kumi la kwanza kwa watu wa Karbala, nazo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeandaa mkakati madhubuti wa mwezi wa Muharam na Safar utakao tangazwa hivi karibuni, maafisa usalama wa mkoa wa Karbala wameimarisha ulinzi na usalama kwa mazuwaru watukufu ndani ya mwezi wa Muharam kwa kushirikiana na kikosi cha Furaat Ausat.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: