Kwa uhudhuriaji wa ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu: Ratiba ya kongamano la Ghadiir katika haram ya Amirul Mu-uminina (a.s) yaanza…

Maoni katika picha
Ratiba ya kongamano la Ghadiir imeanza kutekelezwa katika malalo ya Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa saba, ambalo husimamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu kufuatia kumbukumbu ya siku ya Ghadiir, na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Ataba tukufu na mazaru takatifu pamoja na wawakilishi wa ofisi za Maraajii Dini wakuu, na jopo la walimu na wanafunzi wa hauza na wasomi wa kisekula sambamba na waandishi wa habari na kundi kubwa la mazuwaru watukufu.

Kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Shekh Shabbir Mullah, kisha katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Muhandisi Yusufu Sheikh Raadhi akawasilisha ujumbe wa uongozi mkuu ambao alianza kwa kusema: “Amma baad, Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake kitukufu: (Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufukisha ujumbe wake..), kisha ikaja aya tukufu isemayo: (Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini), akazungumzia mazingira ya tukio la Ghadiir kua linaonyesha kulikua na jambo kubwa ambalo bila kufanyika Dini isinge kamilika, na jambo hilo ndilo alilotangaza Mtume siku hiyo, hapa tunapata swali, siku ya Ghadiir ina nafasi gani?

Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya akaendelea kusema: “Siku ya Ghadiir ni siku ya kutangazwa serikali ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu ambayo ndio lengo la kuwepo na kielelezo cha ukamilifu wake, ndio maana katika ulimwengu wa malaika inaitwa siku ya kielelezo na ahadi iliyo ahidiwa”.

Kisha ukafuata ujumbe wa kiongozi wa wakfu Shia Mheshimiwa Sayyid Alaa Mussawi, ulio wasiliswa kwa niaba yake na Dokta Haidari Sahlaani, akasema kua: “Madhumuni ya hadithi ya Ghadiir yalikua sio mageni kwa Answari na Muhajirina wengi ambao walikua wamesha sikia mara nyingi kutoka kwa Mtume akisisitiza ukhalifa wa Ali na uongozi wake kwa waumini baada yake katika sehemu nyingi na matukio mbalimbali”.

Akasisitiza kua: “Hakika utukufu wa siku hii na yaliyo jiri kwa Ali (a.s) na watu wa nyumbani kwake waislamu hawatofautiani, jambo hili mkanushaji na muungaji mkono wote wanakubaliana”.

Kisha ukafuata ujumbe wa Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Bahrul Uluum ambaye alisisitiza kua: “Toka mwanzoni mwa utume hadithi zinataja fadhila baada ya fadhila na utukufu wa Ali bun Abu Twalib (a.s), na Ghadiir ilikua ni kilele cha hitimisho wa utukufu ulio kua umesha elezewa na hadithi kuhusu Ali na ili iwe hoja ya wazi kwa waislamu wote, ya kwamba Mtume mtukufu (s.a.w.w) alilichukua kiapo cha utii kwa watu, kisha akachukua kiapo kwa waumini cha kumtii Ali bun Abu Twalib (a.s), jambo hili waislamu wote wanalikubali, na lilifanyika ili asipatikane mtu wa kuomba udhuru (wa kudai alikua hajui)”.

Kisha ukaingia wakati wa Dokta Abdulhussein Abudi na kaswida yake kuhusu tukio hili, ambapo alisoma beti za kumsifu kiongozi wa waumini (a.s) halafu kikaingia kikosi cha waimbaji cha Atabatu Alawiyya tukufu ambacho pia kiliimba kaswida zinazo onyesha mapenzi kwa kiongozi wa waumini (a.s) katika siku hii tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: