Jeduali hilo limebainisha kua kiwango cha ung’aaji wa mwezi kitakua cha (%1.25), kwa kiwango hicho unatarajiwa kuonekana kwa macho moja kwa moja kama anga likiwa safi, kwa hiyo inatarajiwa siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam itakua siku ya Juma Nne sawa na (11 Septemba 2018m).
Miongoni mwa matukio ya kidini katika mwezi wa Muharam ni:
- - Mwezi mosi Muharam: Ni mwanzo wa mwaka wa Hijiriyya 1440h / Vita ya Dhaati Riqaai.
- - Mwezi pili Muharam: Kuwasili kwa Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala mwaka wa (61h).
- - Mwezi tatu Muharam: Kufika kwa Omari bun Saadi bun Abu Waqaasi pamoja na jeshi la watu wa Kufa katika ardhi ya Karbala (61h).
- - Mwezi saba Muharam: Kuzuiliwa kupata maji watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika ardhi ya Karbala.
- - Mwezi tisa Muharam: Ujio wa Shimri bun Dhiijaushen na barua ya Ibun Ziyadi (laana iwe juu yao) iliyo agiza kuuliwa Hussein (a.s).
- - Mwezi kumi Muharam: Kumbukumbu ya siku ya Ashura (vita ya Twafu) kuuawa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba zake.
- - Mwezi kumi na moja Muharam: Kuchukuliwa mateka wanafamilia watukufu (watu wa nyumba ya Mtume) na kupelekwa katika mji wa Kufa baada ya vita ya Twafu katika ardhi ya Karbala.
- - Mwezi kumi na mbili Muharam: Kuwasili mateka katika mji wa Kufa.
- - Mwezi kumi na tatu Muharam: Kuzikwa mashahidi wa Twafu (Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake –a.s-).
- - Mwezi kumi na tisa Muharam: Kuondoka msafara wa mateka watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kutoka katika mji wa Kufa kwenda Sham (61h).
- - Mwezi ishirini na tano Muharam: Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali bun Hussein (a.s) mwaka wa 95h / vita ya Qadisiyya mwaka wa (14h).