Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu atembelea familia za wahanga wa maandamano kuwapa pole na aonyesha kua pamoja nao…

Maoni katika picha
Katika matembezi ya vikao vya dua (khitima) vinavyo fanywa kuwarehemu waliouawa katika maandamano ya Basra ya watu wanaodai haki zao, mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alasiri ya Alkhamisi (6/9/2018m) alitembelea vikao hivyo vinavyo fanyika katika mkoa wa Basra.

Mwandishi wa mtandao wa kimataifa Alkafeel amesema kua: “Hakika Sayyid Swafi aliifikishia salamu za rambirambi kutoka kwa Marjaa Dini mkuu kwa kila familia iliyo fiwa, na akaonyesha kushikamana kwake pamoja nao, kwa kumuwakilisha Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Siatani”.

Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu siku ya Juma Pli ya tarehe mbili mwezi huu wa tisa alimuagiza mwakilishi wake Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na jopo la wataalamu waende Basra kuangalia namna ya kutatua tatizo la maji katika mji huo. Sayyid Swafi alipo wasili Basra alisema kua: “Tumeagizwa na Mheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani kutekeleza jukumu maalumu, lano ni kusaidia kutatua tatizo kubwa la watu wa Basra la ukosefu wa maji, tunaendelea kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na muda mrefu, tunafanya kazi kwa vitendo kadri ya uwezo wetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: