Marjaa Dini mkuu: Raia wa Iraq hawawezi kuendelea kuwavumilia viongozi, hakika ufisadi na huduma mbaya ni sababu ya matokeo mabaya…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amebainisha kua raia wa Iraq hawawezi kuendulea kuwavumilia viongozi, hakika ufisadi na huduma mbaya ni sababu ya matokeo mabaya.

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (26 Dhulhijja 1439h) sawa na (7 Septemba 2018m) iliyo swaliwa katika uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Marjaa Dini mkuu anafuatilia kwa karibu yanayo endelea katika mji kipenzi wa Basra, anaumizwa sana na yanayo endelea sambamba na kusikitishwa na mambo yanayo endelea huko, amekwisha tahadharisha zaidi ya mara moja, lakini kwa masikitiko makubwa hakuna aliye zingatia tahadhari hizo, na leo tunarudia kuongelea mambo yafuatayo:

Jambo la kwanza: Tunasisitiza kutokubaliana na kulaani vikali mambo waliyo fanyiwa waandamanaji kwa amani ya kuwashambulia na kuwapiga risasi, jambo lililo pelekea kuuawa waandamanaji kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa, pia tunalaani vikali kushambuliwa kwa vikosi vya usalama vilivyo pewa jukumu la kulinda majengo na mali za serikali kwa kuwatupia mawe na vioo na vitu vingine, jambo lililopelekea kujeruhiwa makumi ya askari, pia tunalaani kushambulia mali za umma na mali binafsi kwa kuzichoma, kuzivunja au kupora na vinginevyo.

Hakika vitendo hivyo, pamoja na kua havikubaliki kisheria lakini pia ni kuongeza tatizo jipya na kuzuia kutatua matatizo yanayo lalamikiwa na wananchi kwa sasa, kupitia mimbari hii tunazitaka pande zote kutotumia nguvu, hasa wakati wa kukabiliana na waandamanaji, vilevile waandamanaji waache kuharibu mali za umma na za watu binafsi.

Jambo la pili: Hakika raia wa Iraq wadhulumiwa, walio vumilia muda mrefu matatizo mengi waliyo pata baada ya kuanguka utawala ulio pita, walishambuliwa kinyama na kusababisha uwepo wa malaki ya wajane na mayatima, kisha wakajitolea watoto wao kuilinda Iraq na maeneo matakatifu katika vita kali iliyo chukua muda mrefu wakipambana na magaidi wa Daesh, wamevumilia mambo mengi kwa muda wa miaka kumi na tano, wakiwa na matarajia kua serikali mpya zitaboresha hali na kua tofauti na zamani, watabata maisha mazuri yenye amani na utulivu, raia hawa wavumilivu hawawezi tena kuendelea kuvumilia kupuuzwa na viongozi wa serikali na kutoona juhudi zozote zikifanywa na serikali za kutatua matatizo sugu waliyo nayo, bali viongozi wanaendelea kuzozana wao kwa wao na kujinufaisha kisiasa katika kugawana madaraka ya serikalini na kuruhusu wageni kuingilia swala la kitaifa na kulifanya jambo la mivutano ya kikanda na kuliweka katika agenda za malumbano ya watu wa nje.

Jambo la tatu: Hakika matatizo ya watu wa Basra na katika mikoa mingine ya ukosefu wa huduma za msingi na kuenea ufakiri na ukosefu wa ajira pamoja na kuenea ufisadi katika ngazi tofauti za serikali, ni jambo la kawaida kwa utendaji mbaya wa viongozi wenye nafasi muhimu katika serikali zote, zilizo undwa kisiasa na ambazo haziangalii uwezo na vigezo vya uteuzi wa viongozi, hasa katika sekta muhimu za kiutumishi, hali hii mbaya haiwezi kubadilika ikiwa serikali ijayo itaundwa kwa mfumo huo huo ulio tumika kuunda serikali zilizo pita, hapa unaonekana umuhimu wa kuhakikisha serikali mpya inakua tofauti na serikali zilizo pita, uangaliwe uwezo, usafi (kutokua na tuhuma za ufisadi), ushujaa, moyo na uzalendo kwa taifa na raia katika kuteua viongozi wakuu wa serikali.

Jambo la nne: Kutokana na ufuatiliaji wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa tatizo la maji katika mji wa Basra imedhihirika kua, sababu za mapungufu ya serikali ya kuto tatua tatizo hilo kwa muda mrefu, wakati ingeweza kutatua tatizo au kulipunguza kwa kiasi kikubwa na kwa nguvu ndogo, inatokana na kutokua na uwezo kwa baadhi ya watendaji wa serikali, huku wengine wakiwa hawajali matatizo ya raia na kutokuwepo na ufuatiliaji stahili katika ngazi husika, mabo hayo yamepelekea tatizo kua kubwa. Hakika ni muhimu sana wenye madaraka katika sekta ya ufuatiliaji watekeleze majukumu yao hasa katika miradi muhimu inayo gusa nyumba za watu, wanatakiwa kuwa na maamuzi ya haraka na yenye tija, kwa mujimu wa maoni ya jopo la wataalamu, sio kuacha mambo yakiwa yanaelea elea baina wa viongozi, au kutumia zana duni zinazo weza kuchelewesha ukamilishaji wa kazi, kazi ambayo ingekamilika ndani ya miezi sita inafanywa kwa miaka kadhaa.

Jambo la tano: Hakika utatuzi wa matatizo mengi unahitaji muda, ni vigumu kuyatutua yote kwa muda mfupi, lakini lazima viongozi waonyeshe wazi uchukuaji wa hatua za kutatua matatizo, ili wananchi wapate matumaini ya kutatuliwa matatizo yao, itasaidia kutuliza nafsi na kupunguza mizozo, jambo linalo saidia katika hili ni viongozi wakubwa wa serikali, mawaziri na wengine wafike sehemu ya tukio na wasimamie utendaji wao wenyewe, na wasikilize moja kwa moja madai ya wananchi, na waonyesho utayari wao wa kuyatatua haraka iwezekanavyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: