Maoni katika picha
- - Mimi nimekuja katika mji huu kwa kuagizwa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani baada ya kuwepo kwa tatizo la maji safi ya kunywa na matumizi mengine ya kibinadamu.
- - Nimekuja kutekeleza jukumu maalumu, baada ya kufanya uchunguzi tumebaini matatizo na mahitaji kadhaa.
- - Mji wa Basra unahitaji mambo mengi, mji huu kipenzi unamatatizo makubwa, wala sio matatizo ya juu juu au mepesi.
- - Mji huu unahitaji utashi wa dhati wa serikali na kukata mizizi ya ufisadi, matatizo haya mawili yapo kwa kiasi kikubwa sana katika mji wa Basra.
- - Unapo ongea na watu wa mji huu, utawakuta wako wazi wana roho nzuri na wazalendo, wanaupenda sana mji wao, wamejitolea kwa ajili ya mji wao –kama ilivyo kwa wakazi wa miji mingine- sitaki kusema kitu kipya, kwa kweli huu ni mji wa mashahidi.
- - Mji huu unatakiwa kupewa umuhimu mkubwa na kila mtu.
- - Baadhi ya watu wanaweza kusema kua kuna miradi, mimi sikatai lakini iko wapi miradi hiyo? Kwa nini baadhi ya miradi inachukua muda mrefu?
- - Mimi nilitambua tatizo pamoja na jopo la wataalamu lililopo, kuna kituo hakifanyi kazi nacho ni kituo cha Aariziru, kikiwa na matatizo matatu, kutokuwepo maji yanayofika kwenye kituo, kutofanya kazi kwa mitambo ya kusukuma maji na kutounganika kwa mitambo.
- - Baada ya kumuambia Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu tatizo la mitambo ya kusukuma maji alituruhusu kununua, tumenunua mitambo hiyo kwa pesa ya Marjaa Dini mkuu.
- - Sasahivi kuna kundi linashirikiana na watu wa Basra pamoja na wataalamu nilio kuja nao wanaendelea na kazi ya ufungaji wa mitambo hiyo, matunda ya mitambo hiyo yataonekana na kuwafikia raia wa kawaida wa Basra, mitambo hiyo itapunguza sehemu ya tatizo.
- - Tumeongea na baadhi ya watu na kuonyesha masikitiko yetu kwao, sisi tunataka kufanya kazi, tulipo baini tatizo asubuhi, Alasiri tukanunua mitambo wa kusukuma maji, jambo hili halihitaji kujadiliana sana hasa baada ya kutambua tatizo.
- - Uzembe na kuacha kutilia umuhimi mambo ni tatizo kubwa litakalo tusumbua.
- - Narudia kusema kua Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani amenipa jukumu maalumu nalo ni kutatua tatizo la maji safi ya kunywa, tumechunguza tatizo hilo na alhamdu lilahi tumeanza kulitatua, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu mtukufu ndugu zetu wataona matunda ya kazi hii baada ya siku chache.
- - Tumefanyia uchunguzi matatizo mengine pia, lakini utatuzi wake upo mikononi mwa ya vyombo vingine vya serikali, nasema: Ikiwa kweli kuna utashi wa kutatua matatizo basi ndugu zetu wafanye haraka kuyatatua.