Kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Unapo andama mwezi wa Muharam Malaika hutandaza kanzu ya Hussein (a.s) ikiwa imelowa damu, sisi na wale wanao tupenda huiona kwa moyo sio kwa macho, huishi katika mazingira yetu nafsi zetu huhuzunika..).
Kutokana na kauli hiyo, huzuni imeanza kutanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajiandaa kutangaza maombolezo katika kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume na kipenzi cha moyo wake Abu Abdillahi Hussein (a.s), kitengo cha uangalizi wa haram cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya maandalizi rasmi ya kuupokea mwezi wa Muharam, miongoni mwa maandalizi hayo ni kudhihirisha muonekano wa huzuni, tangu siku kadhaa wameanza kuweka mapambo meusi katika eneo la uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuandaa mambo mengine yanayo endana na upokezi wa mwezi huu wa huzuni, sambamba na kuandaa mazingira muwafaka ya mazuwaru watukufu watakaokuja Karbala kuomboleza msiba huu.
Vitambaa na mabango yanayo ashiria kuomboleza yameshonywa na kudariziwa katika idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kuchukua vipimo vyote vya lazima katika maeneo ya uwanja wa haram tukufu, sehemu za majengo, kuta na milangoni, waliandaa kiwango kikubwa cha vitambaa vya kifahari kwa ajili ya kazi hii ambayo imechukua muda mrefu.
Kama kawaida yake katika kila mwaka, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kuomboleza, inayo husisha vipengele vingi, utowaji wa mihadhara ya Dini, ufanyaji wa majlis maalumu za kuomboleza tukio hili, baada ya swala ya Magharibi na Isha (siku ya kuandama mwezi) itabadilishwa bendera ya kubba tukufu, pia wametangaza kujiandaa kupokea mawakibu (vikundi) vya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala.