Idhaa ya Alkafeel ya wanawake yawasha mshumaa wake wa kumi na moja…

Maoni katika picha
Idhaa ya Alkafeel sauti ya mwanamke wa kiislamu chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imewasha mshumaa wake wa kumi na moja, kufuatia tukio hilo idara ya idhaa imefanya hafla katika kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s).

Kiongozi wa Idhaa bibi Riayi Ali alizungumza katika hafla hiyo, alianza kwa kuwapongeza watumishi wa Idhaa kutokana na utendaji wao mzuri, akabainisha kua: “Hakika Idhaa imeweza kujijengea uwaminifu kwa wasikilizaji na kufungua milango ya majadiliano na kulea fikra”, akasema kua: “Mitandao ya kijamii inachuana na vyombo vya habari kutokana na uharaka wake wa kuzifikia habari na kuondoa umbali wa kijografia, hivyo viongozi wa vyombo vya habari wanatakiwa kufanya juhudi kubwa itakayo linda heshima na misingi ya habari”.

Mwishoni mwa ujumbe wake akatangaza “Kuanza kwa mradi wa kituo cha Alkafeel wa kuongoza familia, mradi ambao ni kiunganishi kati ya mwanamke na matatizo anayo yapata katika familia pamoja na wabobezi wa ushauri wa kifamilia na tiba ya nafsi”.

Baada ya hapo wakatangazwa washindi wa shindano la (Rahiiqu Almunajaat) ambalo ni shindano la kielimu na kimalezi lililofanywa na Idhaa. Tulifanya mahojiano na mtangazaji bi Zaharaa ambaye ni mwendeshaji wa kipindi hicho katika Idhaa ya Alkafeel pembeni ya hafla na akabainisha kua: “Hakika utangazaji una vikwazo vingi, lakini kwa kua tumesoma katika madrasa ya Alkafeel, madrasa ambayo inamasomo mengi ambayo yanaendelea kutusaidia katika utendaji wa kazi, tunaingia mwaka mpya tukiwa na Idhaa ya Alkafeel ndani ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tukiwa na ratiba bora kabisa ya utangazaji, kila mwaka tunawatakia heri elfu (heri na baraka za mwaka mpya)”.

Bi Ma-Aathir Twalib ambaye ni mtangazaji kutoka taasisi ya Ain aliongeza kusema kua: “Hakika uzowefu wa Idhaa ya Alkafeel unaonyesha kulenga tabaka maalumu katika jamii nalo ni tabaka la wanawake, malengo ya wanahabari wa leo yanasababisha wanahabari wajitenge na baadhi ya mambo, mwanahabari anatakiwa kuzingatia ujumbe wa habari ili kuifanya Idhaa ya Alkafeel iguse mambo yote ya kifamilia na iwe ni sauti ya matatizo ya kifamilia na tegemeo la mwanamke”.

Kumbuka kua Idhaa ya Alkafeel imefungua milango ya mawasiliano na ushirikiano na taasisi za kijamii na vikundi mbalimbali vya wanawake vinavyo fanya kazi ya kuendeleza wanawake kwa lengo la kuendeleza jamii ya wairaq kwa ujumla, mambo ambayo matokeo yake yataonekana moja kwa moja katika jamii, kwa maelezo zaidi kuhusu Idhaa na ratiba zake unaweza kutembelea toghuti ifuatayo: https://alkafeel.net/radio/.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: